Mh Jamali Malinzi,
Nashukuru kwa majibu yako, ila bado nina maswali haya kutokana na majibu yako.
1) Kwanza kwa faida ya kadamnasi nilikuwa naomba nikukumbushe tu kwanza , hujajibu swali kuhusu OKWI, je ni kuwa TFF haina imani na ICT, au kuna ICT za kughushi? Au hamuamini huo mtindo nyinyi uongozi mpya. Nasema hivi ili watanzania wote uweze kutuelewesha, ili kuondoa hoja inayoendelea mtaani kuwa mnafanya kazi kwa kupitia habari zinazoandikwa magazetini.
2) Nikirudi kuhusu kuwa na Timu ya Taifa yenye mafanikio, wewe ni engineer, ingawa ulihitimu siku nyingi, lakini nina imani mpaka leo bado unakumbuka Statistics, na umuhimu wake katika utafiti ili kupata majibu yaliyo sahihi.
Sasa takwimu za nchi ulizonipa hivi kweli wewe zinakupa majibu kuwa hilo ndo jibu la matatizo ya kukosa timu imara Tanzania yenye mafanikio?
Ok, chukulia Zambia as a case study, je umefuatilia kwa undani ni jinsi gani walianza kujenga timu hiyo?
Naomba niishie hapa wakati nasubiri majibu, na niwie radhi kukuchosha kwa maswali.
Ndugu zangu kwa nia njema kabisa ya kujenga nimeamua kutumia muda kujibu maswali na kupokea ushauri.Ninaomba tuulize maswali na kutoa ushauri wa kujenga.Ninaomba tusiongelee watu tuongelee issues,tuangalie ni kwa jinsi gani tutakabiliana na changamoto mbali mbali.
Kuhusu ligi kuwa na timu zaidi ya 14 ni kweli tumeliona na tutashauriana na mshirika wetu vodacom ili tuone tutafanya nini.
Me Naomba Nitoe Ushaur Kwa Tff. Niliona Video Ya Jkt Kanembwa Na Stand United Ki Ukwel Bila Kupepesa Macho Wala Kung'ata Maneno Stand United Mtaionea Hata Kama Mech Itapangwa Kuchezw Shnyanga, Kwasababu Refa Altoa Penalt Kanembwa Wakagomea Wakamzonga Refa Na Intention Ilkua N Kumpga 2naamin Maamuz Ya Mwisho N Ya Refa Sasa Kwann Kanembwa Wamzonge Mwamuzi?
Naona mh. Unaongelea soka la vijana na football academy, lakini huko ni mbali saana kwa nini msijihusishe na Umitashumta na Umisseta, pia unalalamikia uchache wa makocha kwa nini msitoe kozi na semina kwa walimu wa msingi na sekondari??? Ni rahisi Kwetu zaidi kuwafundisha mpira vijana tunaowafundisha darasani.
Kumekuwa na kozi zinatolewa lakini zinatolewa kiundugu zaidi... Pia ktk copa coca cola kuna upuuzi mwingi sana hasa huku mikoani, hebu fuatilia Hilo. Ningekushauri ongea na viongozi wa TAHOSSA uone jinsi gani unaweza wahusisha walimu ktk kufundisha mpira... Kama tunaweza kumfundisha akajua kusoma!! Kwa nini tushindwe kumfundisha kucheza mpira??? Fani ya ukocha mmeifanya ya waganga njaa!! Tupeni walimu skills kidogo tuchanganye na zetu muone
Lengo letu ndilo hilo tunataka vyuo kama malya,butimba,murutunguru wahitimu wake licha ya kupewa vyeti vya kuhitimu vya kawaida lakini pia watoke na CAF coaching licenses.
Jamal Malinzindugu yetu Malinzi ombi langu kwa TFF ni kuongeza timu za ligi kuu kutoka 14 zifike angalau 18 au 20 ili kuleta ushindani na kuzifanya timu zicheze mechi nyingi zaidi.
Hahaha...ukipata jibu uniambie na mmHivi rufaa ya Serengeti boys dhidi ya kijeba cha Congo-Brazzaville imeishia wapi?
Mhh, nalisikia kulikuwa na ujumbe maalum wa TFF umepiga kambi kule Cairo kufuatilia hilo suala. Ila naona kimyaa na hakuna mrejesho, sijui wamerudi au bado wanaendelea kula bhata za kiarabu!!Hivi rufaa ya Serengeti boys dhidi ya kijeba cha Congo-Brazzaville imeishia wapi?