Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

Swali: ni kweli kuwa Wakuu wengi wa Idara, TFF ni Wahaya wenzako??????
 
Hongera kwa kusaini mkataba wa kutandika nyasi bandia uwanja wa nyamagana mwanza, Je kuna mpango wowote wa kujenga majukwaa? mimi nafikiri kwa sababu uwanja huo hautakuwa olimpiki style (yaani kuwa na michezo mingine kama riadha n.k) nafikiri eneo linatosha kabisa kujenga majukwaa, anzisheni ligi ya vijana yaani miaka 17 na kuendelea inachezwa kikanda halafu kitaifa, ili kuipa msisimko ligi hiyo timu inayokuwa bingwa inapata nafasi ya kwenda ligi daraja la kwanza, mashindano yaanze ngazi ya mkoa kwa maana ya kila wilaya kushiriki baadaye kikanda kisha kitaifa, ni ushauri tu ninatoa. Naongea hivi kwa sababu wakati pamba inawika mara nyingi ilikuwa ikichukua vijana wengi kutoka mashindano ya shule za sekondari za mwanza yaliyokuwa yakidhaminiwa na lions club kama sikosei, asikwambie mtu mwanza ilikuwa inazizima hayo mashindano yakianza utadhani nini sijui, na kulikuwa kuna watu wana vipaji acha tu, kitafutwe kitu cha kurudisha msisimko maana miaka hiyo mwanza ilikuwa na watu kama laki nne hivi lakini mechi za pamba uwanja wa kirumba unajaa, sasa hivi mwanza ina watu karibu milioni moja lakini ukienda uwanjani aibu watu waliopo,jaribuni kuvihamasisha vyama vya mikoa kujivunia timu zao ili kuleta msisimko kama wafanyavyo mbeya city, muwape mikakati na muwabane watz huwa hatufanyi vitu bila kubanwa, ni hayo tu kwa leo nina mengi ya kuadvise lakini mvivu kuandika

swali.... je hamuwezi kuongea na mashirika kama nssf, ppf, tbl, pspf, na mengine yenye uwezo ili vijengwe viwanja vikubwa kama cha dar kwa kila kanda? hii itasaidia hata moja ya timu za kanda husika inapochukua inapopata nafasi kushiriki mashindano makubwa kutokuwa mbali na mashabiki wake kama ilivyowahi tokea kwa timu kama prisons ilipohamia dar? au kama hilo ni haliwezekani basi wawafadhili ili mtandike nyasi bandia kila kiwanja kikubwa cha kila mkoa, na kwa sababu viwanja vingi ni vya ccm basi mkae nao ili muone kama mnaweza kuvimiliki nyie.

Kuna watu wa sunderland wanataka kujenga kiwanja dar, hatuwezi kuwashauri hiyo shule angalau waijengee morogoro ili kuondoa utitiri wa viwanja vizuri kuwa dar tu? kama morogoro wataona mbali basi hata pwani.
 
Mh Jamali Malinzi,

Nashukuru kwa majibu yako, ila bado nina maswali haya kutokana na majibu yako.
1) Kwanza kwa faida ya kadamnasi nilikuwa naomba nikukumbushe tu kwanza , hujajibu swali kuhusu OKWI, je ni kuwa TFF haina imani na ICT, au kuna ICT za kughushi? Au hamuamini huo mtindo nyinyi uongozi mpya. Nasema hivi ili watanzania wote uweze kutuelewesha, ili kuondoa hoja inayoendelea mtaani kuwa mnafanya kazi kwa kupitia habari zinazoandikwa magazetini.

2) Nikirudi kuhusu kuwa na Timu ya Taifa yenye mafanikio, wewe ni engineer, ingawa ulihitimu siku nyingi, lakini nina imani mpaka leo bado unakumbuka Statistics, na umuhimu wake katika utafiti ili kupata majibu yaliyo sahihi.

Sasa takwimu za nchi ulizonipa hivi kweli wewe zinakupa majibu kuwa hilo ndo jibu la matatizo ya kukosa timu imara Tanzania yenye mafanikio?

Ok, chukulia Zambia as a case study, je umefuatilia kwa undani ni jinsi gani walianza kujenga timu hiyo?

Naomba niishie hapa wakati nasubiri majibu, na niwie radhi kukuchosha kwa maswali.

1.suala la Okwi tutapewa mwongozo na FIFA muda wowote na kwa kuwa kuna masuala ya kisheria nisingependa kuongelea sana.
2.Youth programme ya Zambia inasimamiwa na serikali toka enzi za Kaunda.Zambia vipaji vinapatikana shuleni na serikali ina foot bill zote za timu za taifa za vijana.Nimeongea na Kalusha Bwalya kanithibitishia hili.Tanzania mpaka TFF ijikongoje ndo iingize timu za taifa kambini za U17,U20 girls and boys na Twiga stars,tafakari kisha unipe jibu.
 
1@ngokongosha pamoja na kwamba mimi sio msemaji wa wamiliki wa nyamagana ambao ni manispaa lakini nikufahamishe tu kuwa majukwaa yatajengwa.
2.Mradi wa Symbion/Sunderland una wasimamizi wake na serikali imekwisha utengea maeneo.Muhimu mashirika mengine nayo yakaiga.
3.Ni kweli Mwanza na utajiri wake sio wa kuwa kuwa hivi kimpira.
 
Ndugu zangu kwa nia njema kabisa ya kujenga nimeamua kutumia muda kujibu maswali na kupokea ushauri.Ninaomba tuulize maswali na kutoa ushauri wa kujenga.Ninaomba tusiongelee watu tuongelee issues,tuangalie ni kwa jinsi gani tutakabiliana na changamoto mbali mbali.
Kuhusu ligi kuwa na timu zaidi ya 14 ni kweli tumeliona na tutashauriana na mshirika wetu vodacom ili tuone tutafanya nini.

Naona mh. Unaongelea soka la vijana na football academy, lakini huko ni mbali saana kwa nini msijihusishe na Umitashumta na Umisseta, pia unalalamikia uchache wa makocha kwa nini msitoe kozi na semina kwa walimu wa msingi na sekondari??? Ni rahisi Kwetu zaidi kuwafundisha mpira vijana tunaowafundisha darasani.
Kumekuwa na kozi zinatolewa lakini zinatolewa kiundugu zaidi... Pia ktk copa coca cola kuna upuuzi mwingi sana hasa huku mikoani, hebu fuatilia Hilo. Ningekushauri ongea na viongozi wa TAHOSSA uone jinsi gani unaweza wahusisha walimu ktk kufundisha mpira... Kama tunaweza kumfundisha akajua kusoma!! Kwa nini tushindwe kumfundisha kucheza mpira??? Fani ya ukocha mmeifanya ya waganga njaa!! Tupeni walimu skills kidogo tuchanganye na zetu muone
 
Me Naomba Nitoe Ushaur Kwa Tff. Niliona Video Ya Jkt Kanembwa Na Stand United Ki Ukwel Bila Kupepesa Macho Wala Kung'ata Maneno Stand United Mtaionea Hata Kama Mech Itapangwa Kuchezw Shnyanga, Kwasababu Refa Altoa Penalt Kanembwa Wakagomea Wakamzonga Refa Na Intention Ilkua N Kumpga 2naamin Maamuz Ya Mwisho N Ya Refa Sasa Kwann Kanembwa Wamzonge Mwamuzi?
 
Kamati ya utendaji ya TFF imeiagiza bodi ya ligi kupitia upya kesi hii ili haki ionekane imetendeka.Aidha kamati ya nidhamu nayo itakutana jumatano kushughulikia kipengele cha nidhamu kwa watovu wote.
 
Naona mh. Unaongelea soka la vijana na football academy, lakini huko ni mbali saana kwa nini msijihusishe na Umitashumta na Umisseta, pia unalalamikia uchache wa makocha kwa nini msitoe kozi na semina kwa walimu wa msingi na sekondari??? Ni rahisi Kwetu zaidi kuwafundisha mpira vijana tunaowafundisha darasani.
Kumekuwa na kozi zinatolewa lakini zinatolewa kiundugu zaidi... Pia ktk copa coca cola kuna upuuzi mwingi sana hasa huku mikoani, hebu fuatilia Hilo. Ningekushauri ongea na viongozi wa TAHOSSA uone jinsi gani unaweza wahusisha walimu ktk kufundisha mpira... Kama tunaweza kumfundisha akajua kusoma!! Kwa nini tushindwe kumfundisha kucheza mpira??? Fani ya ukocha mmeifanya ya waganga njaa!! Tupeni walimu skills kidogo tuchanganye na zetu muone

Lengo letu ndilo hilo tunataka vyuo kama malya,butimba,murutunguru wahitimu wake licha ya kupewa vyeti vya kuhitimu vya kawaida lakini pia watoke na CAF coaching licenses.
 
ndugu yetu Malinzi ombi langu kwa TFF ni kuongeza timu za ligi kuu kutoka 14 zifike angalau 18 au 20 ili kuleta ushindani na kuzifanya timu zicheze mechi nyingi zaidi.
 
Vipi kuwa na ligi ya kulipwa...hii mshawahi kulijadili..au hata kuwepo ktk mipango yenu
 
Lengo letu ndilo hilo tunataka vyuo kama malya,butimba,murutunguru wahitimu wake licha ya kupewa vyeti vya kuhitimu vya kawaida lakini pia watoke na CAF coaching licenses.

Kila lakheri kamanda
 
ndugu yetu Malinzi ombi langu kwa TFF ni kuongeza timu za ligi kuu kutoka 14 zifike angalau 18 au 20 ili kuleta ushindani na kuzifanya timu zicheze mechi nyingi zaidi.
Jamal Malinzi

kwahili twende taratibu,
tuongeze zifike 16 then 18 then 20. na sio haraka haraka.

pia isije ikaw mambo ya kuw amwaka huu hakuna kushuka daraja, hatutaki kusikia hili ni bora kuboresha ligi daraja la kwanza na kuhakikisha badala ya kupanda watu wawili wapande wanne lakini kushuka wawili kila mwaka ni lazima.
 
Last edited by a moderator:
Invisible

Tafadhali Unaganisha huu na ule pale juu, Ila kuwa makini kuna Maswali kule hayajajibiwa usija ukayafunika. Nadhani unaweza kuweka huu uzi kuanzia Post number Mbili katikati hapo.
Ila ya kwanza ikabaki ya Mheshimiwa Malinzi. Na pia kuna Haja ya Kubadilisha heading kule ili neno TFF liwepo maana sio wadau wote wanao jua Malinzi ni nani na pengine wangependa kuichangia TFF.
 
Last edited by a moderator:
Mimi sina swali.lakini pamoja na mikakati yako unayofanya kwa kipindi kifupi siha imeboreka sana-pongezi...
 
Mkubwa Malinzi kwanza nakupongeza kwa utaratibu huu, nataka kujua kwanini TFF inakuwa na mdhamani mmoja wa Ligi Kuu wakati wenzetu wengine wanakuwa na mdhamani zaidi ya mmoja, sidhani kama Vodacom peke yake anaweza kutosheleza mahitaji ya timu.

Kwa nini TFF isifikikirie kuwa na udhamini wa kusafirisha timu kwenda mikoani na hata hoteli za kufikia sehemu mbalimbali za nchi ili tuweze kuwa na ligi yenye ishindani wa kweli?
 
Malinzi,

Nashukuru kwa kuja hapa na kutoa majibu ya maswali yetu maana sikutegemea kama hata ungeingia kujibu wakati nauliza. big up!

Swali jingine: Je unampango gani na mikoa ambayo haina timu kwenye ligi kuu?

Ushauri: Ndugu Malinzi mimi naomba ukiweza uanzishe ligi nyingine tofauti ambayo haina u-simba na u-yanga. Na sisi tuone mpira wa kiushindani kama wa wenzetu. Ndoto yangu kuona siku moja Ilala United Vs KInondoni Worriors nk
 
Bwana Malinzi haya makato ya mechi lukuki chama cha marefa , chama cha DRFA nk inakuwaje?

Kwani hamuwezi kufanya mabadiliko hivi vyama nk watafute mapato kwa njia tofauti ili timu zipate pesa?
 
Hivi rufaa ya Serengeti boys dhidi ya kijeba cha Congo-Brazzaville imeishia wapi?
 
Hivi rufaa ya Serengeti boys dhidi ya kijeba cha Congo-Brazzaville imeishia wapi?
Mhh, nalisikia kulikuwa na ujumbe maalum wa TFF umepiga kambi kule Cairo kufuatilia hilo suala. Ila naona kimyaa na hakuna mrejesho, sijui wamerudi au bado wanaendelea kula bhata za kiarabu!!
 
Back
Top Bottom