Dah, moja kati ya nyuzi nzuri na yenye sense of patriotism ni hii aisee. Mleta mada kwa kweli uzalendo uliofanya hapa ni wa kiwango cha juu sana. Charity starts at home indeed.
Nami nikuunge mkono katika hili kwa kuamsha hamasa ya kutembelea vivutio vyetu. Tukifanya hivi hakika hata uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla tutaunyanyua haraka sana.
By the way, Nchi yetu ni nzuri sana sana jamani, dah. Hakika tumependelewa sana na Mungu. Lakini kwanini sisi ni masikini hivi??? [emoji24][emoji24]
Anyway labda watu wako makanisani na misikitini wakimwomba Mungu atufungue macho na akili zetu, ili tuone utajiri aliotupatia.
Kwa kweli nimeupenda huu uzi na hakika mimi pia ntaongeza ziara kama mleta mada alivyotuhamasisha. Kwakweli nazikumbuka ziara zangu mbugani Manyara, Ngorongoro, Tarangire, utalii Zanzibar, snake park Arusha, aagh.. zilikuwa ni safari zenye kutuliza akili sana na kukumbukwa daima. Trips of lifetime.
Lakini pia kutalii kunaongeza ufahamu sana. Barikiwa sana mleta mada kwa nyuzi murua kama hii..