Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

44CA2786-AC3A-4A65-88C7-C82ED654EB0D.jpeg
 
DONDOO MUHIMU UNAPOTAKA KUPANGA SAFARI/MATEMBEZI.

Nimeona nishare hii kitu kwaajili ya kusaidia kurahisisha baadhi yetu kutimiza malengo yetu ya kusafiri.

Nianze kwa kusema matembezi (vacations) si kitu cha kufanya tu kwa kukurupuka kama vile unavyoweza kuamka asubuhi na kwenda kwa mama muuza, Vacation ni kitu ambacho kinapangwa na kuwekewa malengo, huwezi kusafiri for no reason, matembezi yanakuja na force fulani from within, hapa ndio tunapata wale wenzangu na mimi unajikuta tu kuna desire fulani tu inakuvuta kupanga matembezi, hiyo power inayokusuma ni jambo muhimu sana katika kufanikisha lengo lako la safari.

Hapa nimekuandalia hatua Tano (5) za kufuata unapotaka kuplan matembezi yako.

Twende sote,

1. Weka lengo/malengo ya kusafiri, wapi unataka kwenda kutembelea.

Hapa ndio mwanzo wa kila kitu, "kupanga ni kuchagua" , ebu set malengo yako ya kusafiri hapa, (set vacation goals), despite una hela au huna we weka malengo tu wapi unataka kwenda. Lakini kwenye malengo kuna vitu vya kuzingatia.

*Lengo la safari
Kwanini unasafiri?
Unataka kwenda kujifunza, unataka kwenda kurefresh tu, unataka kwenda kujipongeza kwa mafanikio fulani ulio ya accomplish kwa kipindi fulani cha mwaka, au unataka tu usafiri ili ukapige picha upost IG na kwenye uzi wa matembezi JF??? [emoji36]
Ukishajua lengo la kusafiri itakupa picha fulani ya wapi upange kutembelea, twende taratibu tu.

*Pocket/Budget
Je maingizo yako ya pesa (source of income) yanakuruhusu kwenda wapi?? You can go anywhere lakini swala la income linachangia hapa so ukizingatia hili utakuwa ushapata picha ya kuchagua wapi nataka kwenda.

Plan na malengo ya vacations huwa yanaanza mapema sanaa, let's say mwanzoni mwa mwaka mtu unaweza kujiwekea malengo kuwa at the end of this year lazima niende serengeti na familia au sikukuu ya pasaka mwaka huu nataka nikaspend saadani hii inakujenga kiakili katika harakati zako za kutafuta unakuwa ushaweka akilini kwamba lazima nijinyime kwaajili ya lengo fulani.


2. CHAGUA MUDA WA KUSAFIRI.

Unaweza ukaona hili halina maana lakini hiki ni kipengere cha muhimu sanaa katika dondoo hizi.
Muda wa kusafiri una faida kwenye ku timing ratiba zako (kutokuingiliana kwa ratiba), lakini muhimu zaidi ni kwamba muda wa kusafiri uta determine hata amount ya pesa utakayospend kwenye vacation yako, kivipi??

Vipindi vya matembezi vimegawanyika kutegemea na

*Seasons
Hapa kuna

High/Peak season

Hiki ni kipindi ambacho watu wengi wanakuwa wanatoka kwaajili ya matembezi mara nyingi yanaangukia vipindi vya holidays let's say mwisho wa mwaka n.k, what you need to know? Kipindi hiki ni kipindi ambacho karibia facilities zote zinakuwa bei juu, kuanzia transport ,accommodation , meals etc so ukipanga vacation kipindi hiki tegemea hilo.

*Low/Off peak season
Hiki ndio kile kipindi cha "fungulia mbwa" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], hapa vitu vingi vinakuwa vimeshuka, hata ukienda kwenye mahoteli makubwa kama Ngurdoto, serena kule serengeti unaweza ukagombaniwa (kidding) kuna kuwa na ukame sana wa wateja, camp sites nyingi zinafungwa kwaajili ya matengezo baada ya kupokea wageni wengi high season lakini pia huwa wanapunguza operation cost kulipa wafanyakazi wakati hamna kazi kwa muda huo. Wajanja na wale wapo sensitive na budget huwa wanasafiri kipindi hiki.

Lakini pia vipindi vya kusafiri vinaweza vikategemea na

*Weather
Hali ya hewa inaweza ikawa factor nyingine ya kupanga kipindi cha kusafiri, hapa kuna vipindi vya mvua, jua na joto, vipindi vya baridi, hapa inategemea unataka nini na kwa muda gani, kama ni mtu wa adventures na hiking wet season utafeel ile nature ya hiking yenyewe na kadhalika.


3. TAZAMA BEI ZA FACILITIES TOFAUTI TOFAUTI KUTEGEMEA NA WAPI UNATAKA KWENDA.

Ingia kwenye mitandao angalia kuna camp sites gani mikumi, au kuna lodge gani saadani angalia bei zao tafuta chaguo ambalo utaona unaweza kuafford kwa muda huo, kama utainclude flights basi cheki nauli ya ndege kwa kipindi fulani itakuwa kiasi gani, kama utakuwa na mahitaji ya kununua kama mountain gears, viatu vya kusafiria ,tents cheki bei zake kabisa, hii itakusaidia kupata ile roughly figure kwamba budget yangu itarange kiasi gani, tunaenda sawa hapo??

4. CHAGUA AGENT.
Hii si muhimu kwa wote, kuna ambao wanapenda kuandaa safari zao wenyewe pasipo kuinclude agent yeyote wa tour, either local or company na wengine wanapenda mambo yawe smooth huwa wanataka kuandaliwa safari interms of itinerary au guide wa kuwaongoza na vitu kama hivyo so ukiona una uhitaji huo anza mapema kuchagua ni agent gani unataka umtumie au utakuwa nae kwenye safari yako, (kuna safari nyingine hazina uhitaji wa tour operator ni wewe na pesa zako tu)


5. ANDAA BAJETI NA WEKA MIPANGO MAHSUSI YA KUSAVE KWA AJILI YA SAFARI YAKO.

Hiki ndio kipengele mama, na lawama nyingi za watanzania huwa zinasukumiwa hapa, uchumi! Uchumi! Uchumi!

Chief, ni bia ngapi unakunywa kwa mwezi?? [emoji23][emoji23][emoji23]

Well tuendelee, ukishachambua hayo yote na kutoka na jibu lako let's say this December i must visit serengeti, hapo umefanya asilimia 30 tu ya safari yako 70% yote inaangukia hapa.

*WORK FOR IT
Kuna vitu tunaweza kujifunza kwa wenzetu wazungu, hili mojawapo, ushawahi kufanya kazi for a certain purposes let's say nafanya biashara hii nikipata faida lazima niende ngorongoro, you know how it feels??? Bruh utafanya kazi/biashara yako kwa bidii tu kwakuwa kuna malengo yako umejiwekea so vacation ifanye iwe lengo kama malengo mengine, kujenga, kununua kiwanja etc.

*SAVE
Kupata pesa inaweza isiwe tabu sanaa je unasave??? Tayari una malengo ushaweka na umefanikiwa kupata lakini kuna changamoto fulani, mtu kakukopa, michango ya harusi. [emoji848], stick on your plans, narudia tena kupanga ni kuchagua. Ikifia mwisho wa mwaka unaenda kujipongeza zako huko mbugani.

Wenzetu wameenda mbali zaidi kuna accounts za vacations tu mtu akiokota pesa anaenda kuitupia tu, nikuahidi ukifuata haya niliyoyaandika hapa, wote december hii tuna enda Dubai [emoji23][emoji23].

Niwatakie mchana mwema.

Karibuni.

Paula Paul Elli Aurora
black sniper mama D Ms mol
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Welcome to lushoto.....
They call it Norway of Africa
Kuna vivutio vingi sana kuanzia safu za milima ya usambara and a lot more

MULLERS mountain Lodge
Swiss Farm
Kigula hakwewa view
.
.
.

.
Soon narudi for more photos

[emoji991] Photos captured my me.[emoji18]
PXL_20230205_120620849.jpg
PXL_20230322_130529738%20(2).jpg
PXL_20230322_130728271.jpg
PXL_20230513_134948370.jpg
PXL_20230325_125451641.jpg
PXL_20230325_113430455.jpg
 
Welcome to lushoto.....
They call it Norway of Africa
Kuna vivutio vingi sana kuanzia safu za milima ya usambara and a lot more

MULLERS mountain Lodge
Swiss Farm
Kigula hakwewa view
.
.
.

.
Soon narudi for more photos

[emoji991] Photos captured my me.[emoji18]
View attachment 2632703View attachment 2632704View attachment 2632705View attachment 2632708View attachment 2632707View attachment 2632706
Weka na bei. Hapo Swiss kila mtu anapaoongelea.

RRONDO nadhani ameenda LUSHOTO ebu kwa 2 nights mtu akiwa na 300k atafaidi nini na nini? ie anafika Ijumaa analala (1st night), jumamos anashinda, analala kuamkia j2 (2nd night,) mida ya mchana anasepa..
 
Weka na bei. Hapo Swiss kila mtu anapaoongelea.

RRONDO nadhani ameenda LUSHOTO ebu kwa 2 nights mtu akiwa na 300k atafaidi nini na nini? ie anafika Ijumaa analala (1st night), jumamos anashinda, analala kuamkia j2 (2nd night,) mida ya mchana anasepa..
Nakazia northbright ebu tupe taarifa za muhimu kuhusu mahali hapo mkuu.
 
Mlima Meru, unavyoonekana maeneo tofauti tofauti katika majira tofauti ndani ya mkoa wa Arusha.

096AC1E0-5473-4E11-941D-C29965BC652E.jpeg
65D3E0CC-68E0-4F98-9E21-666E2B544418.jpeg
10F534BC-73F9-41C9-A311-F8D0F2F75531.jpeg
 
Back
Top Bottom