Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

Kikuletwa is overrated. Ni pazuri sana lakini wizara ya utalii imeshindwa kupaboresha hapo? Je hakuna mwekezaji anaweza kukabidhiwa hiyo sehemu? Barabara ya kutoka boma ng'ombe ufike hapo hot spring ni rough road.

Ukifika pale hamna sehemu ya chakula wala vinywaji inayoeleweka. Hata viti vya kukalia hamna... it's pathetic kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa is overrated or underrated?
Mimi nimesoma shule za kata
 
True say, nadhani ni fursa nzuri pia hata kwa wadau humu JF kuwekeza, nice observation.
 
January nilikuwa tanga muheza na tanga mjini nilifurahi kujionea mazingira mapya katika macho yangu.

Feb nimeplan kuwa bagamoyo sijui hapa ni mahali gani sitakiwi acha kufika kujionea vitu.

kusafiri /kutembelea maeneo ni rahisi ukijiwekea mipango
Well said mkuu,

Kwa bagamoyo, kuna utajiri mkubwa wa utalii wa kihistoria na bahari pia.

Ukifika mjini kabisa unaweza kufika kwenye jengo la "caravan serai" hapa ni jengo lililotumika kupokea watumwa na kuwahifadhi kabla ya kusafirishwa Zanzibar kwaajili ya kuuzwa kwenye mataifa mbalimbali hasa Arabuni,

Pia ukiwa hapo hapo mjini unaweza kutembelea hifadhi ya mji mkongwe wa bagamoyo ambapo utajionea boma la mjerumani lililotumika kama ofisi ya utawala wao, jengo hili lilijengwa mwishoni mwa karne ya 18 na wajerumani.

Pia unaweza kutembelea kanisa kongwe kabisa hapa afrika mashariki ambalo lilijengwa mwaka 1872 kanisa ambalo maiti ya mmisionary muingereza bwana David Livingston ilihifadhiwa kabla ya kusafirishwa kwao uingereza ikitokea Tabora alipofariki. Kanisa hili ni chachu na alama iliyotumika kueneza ukristo katika pwani ya afrika mashariki.

Baada ya hapo unaweza kwenda kutembelea masalia ya kale huko kaole ambapo utajionea magofu na makabuli mbalimbali ya kihistoria huku ukipata upepo murua kutoka katika fukwe ya bahari ya bagamoyo.

Karibu.
 
Ila kufika hapa kwenye kilele cha huu mlima ambapo ndipo kilipo kijiji hiki ni shughuli pevu,ukiwa na gari safi kama land cruiser isiyo na mafua inaweza kukuchukua masaa manne hadi matano kuupanda huu mlima,hapo kijijini maisha ni safi kabisa,utadhani uko mbagala(cunning) kutoka chini ya mlima hadi kijijini(kileleni) kwa pikipiki ni Tsh 30,000/ na kushuka ni 20,000 hadi 15,000,nilipapenda mno.
Gonja mahore,kwa akina Mshana Jr jina la kijiji limenitokaView attachment 1358791

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…