Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

I am very thankful for your write up Mla bata.
Je ni season gani ni nzuri kwa ajili ya kutembelea huko?
Well, asante Paula Paul
Utalii wa magoroto hautegemei sana hali ya hewa au vipindi tofauti tofauti vya majira ya mwaka, kwahiyo naweza kusema unaweza kwenda magoroto anytime.

N:B Changamoto kubwa inaweza kuwa ni barabara kipindi cha mvua kutegemea na aina ya usafiri unaoutumia i.e gari ndogo kama ist na mfanano wake zinaweza kuwa changamoto, ingawa baadhi yetu tunapenda kipindi hiki cha mvua kwaajili ya kwenda kufanya hiking na kufeel nature & adventures.

Karibu.
 
Karibu sanaa Paula Paul ni imani yangu utayapata yote hayo kutoka humu.
Asante kwa thread nzuri. Ni mara chache siku hizi watu wanaanzisha thread za maana kama hizi. Mambo ya utalii sisi waafrika hasa watanzania tupo nyuma sana.

Sidhani kama mara zote fedha ni kikwazo kwani nimeshaona watu wengi wenye uwezo lakini hawatalii. Mimi napenda sana kutalii na kusema ukweli ndoto yangu ni kuitembelea Tanzania yote.
 
Udzungwa ipo wapi?.
Na vivutio gani vinapatikana huko?

Kwa niaba ya mjumbe hapo juu.

Hifadhi ya milima ya Udzungwa ipo nje kidogo ya mji wa morogoro km 65 kusini mwa hifadhi ya taifa ya mikumi, mwendo wa takribani masaa 5 kutoka dar es salaam.

Hifadhi hii ina species takribani 2500 za mimea, species zaidi ya 400 za ndege na specie 11 za nyani ambao ni alama muhimu ya utalii wa udzungwa ikiwemo red colobus and Sanje Crested Mangabey.

Pia Hifadhi ya milima ya udzungwa ina water falls nzuri za kuvutia kama Sanje water falls, prince bernhard water falls etc
 
Asante sana mkuu, umezungumza ukweli mtupu kuhusu ustaarabu wa kutalii kwa sisi waafrika, nadhani ni utaratibu ambao wengi hatuna, labda kupitia nyuzi kama hizi tunaweza kupata wadau watakaopata muamko.
 
Mkuu sasa quotation in united states dollars maana yake nini? Huu ndio tunaita uswahili.
Hiyo ni document iliyoandaliwa kwaajili ya matumizi ya ofisi ambayo wageni ni both waswahili na foreigner.

Nisamehe mimi kwa uswahili wangu mkuu ila dollar moja ni approximately elfu 2280-2300 za kitanzania.

Asante na karibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwamba sijui thamani ya dollar moja kwa shilingi, swali langu why quote in usd?

Mlipaswa in the first place kua na price schedule 2, for locals and foreigners. Locals in tzs na foreigners in usd. Hata tanapa wana hiyo kitu.
 
Sawa asante kwa ushauri.

Sio kwamba sijui thamani ya dollar moja kwa shilingi, swali langu why quote in usd?

Mlipaswa in the first place kua na price schedule 2, for locals and foreigners. Locals in tzs na foreigners in usd. Hata tanapa wana hiyo kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wow, thank you Mla bata. I am always looking for nice hiking recommendations.
Mungu akijalia nitafika huko. Nitakupa na mrejesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…