Uzi wa ushahidi wa mambo ya kusikitisha katika uchaguzi mkuu wa 2020

Uzi wa ushahidi wa mambo ya kusikitisha katika uchaguzi mkuu wa 2020

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2017
Posts
7,101
Reaction score
18,051
Wana JF,

Huu uzi ni wa kumbukumbu. Weka hapa mambo yote ya kusikitisha yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa 2020. JF ni sehemu ya kuelimishana na kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Bila kujali mwelekeo wako kiitikadi, tafadhali weka hapa picha, video, maelezo, ama visa vya mambo mbalimbali ya kusikitisha uliyoyashuhudia ama kuyasikia ya KUSIKITISHA kuhusu uchaguzi wa 27 na 28 Oktoba 2020. Internet imerejeshwa sasa. Lete ma-video, picha, nk ambazo ulipiga lakini haukuweza kutuma kwa kukosa internet.

Kusema ukweli, Mungu ameniwezesha kuona chaguzi zote za vyama vingi tangu 1995 lakini sikupata kuona kura zenye tiki zikibebwa katika mabegi na vikapu kama mwaka huu 2020, zikiingizwa katika vituo vya kupigia kura nchi nzima, chini ya ulinzi wa vyombo vya usalama!

Kulikuwa na visa vya kusikitisha hata kabla ya uchaguzi. Wagombea wa upinzani walienguliwa kwa njia za kimafia kama kutekwa, kukamatwa na kufungwa ili muda wa kurudisha fomu upite, kunyang'anywa fomu kwa nguvu, kushawishiwa kwa pesa, nk.

NEC ina wajibu wa kuwasaidia wagombea katika kujaza fomu lakini iliwatafutia sababu ili kuwaengua. Mathalani, wakati wagombea wengine walienguliwa kwa fomu zao kuwa na jina la chama kama CHADEMA (badala ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO), wengine walienguliwa kwa kuandika CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO badala ya CHADEMA.

Wakati wagombea wengine walienguliwa kwa kujaza CHADEMA kwenye fomu kama jina la chama, NEC ilipotoa fomu ya kupigia kura, iliweka CHADEMA kama jina la chama kwenye fomu hiyo!

Wagombea waliokata rufaa, NEC ilikalia rufaa zao. Wale ambao zilisikilizwa, ilichukuwa zaidi ya mwezi kutoa uamzi! Na uamzi ulipotolewa, wale walioshinda, hawakupewa barua za kushinda rufaa. Na kwa hiyo hawakuruhusiwa kufanya kampeni. Kuna Wakati Mahera aliwaomba Wasimamizi wa Majimbo wawape barua kana kwamba hawawajibiki kwa NEC!

Kuna mgombea ambaye hakuruhusiwa kufanya kampeni baadhi ya mikoa ya kusini japo alikuwa na ratiba hiyo kutoka NEC. Alidanganywa kuwa kulikuwa na kimbunga mikoa hiyo ili asiende huko. Wahudhuriaji katika mikutano yake walipigwa mabomu ya machozi. Kampuni za simu zilizuia taarifa za kumhusu mgombea huyo kutumwa katika mitandao yao!

Wakati wa kampeni, vyombo vya habari vilitangaza habari za mgombea mmoja tu kwa kiasi kikubwa. Na kuhujumu kampeni za wagombea wengine.

Vyombo vya serikali vilihujumu baadhi wa wagombea kwa makusudi kabisa. Feri kati ya Ukerewe na Kisorya, ilikataa kumvusha hyo mgombea wa upinzani. Mamlaka ya Anga ilikataa kutoa kibali cha chombo chake kuruka.

Kuna mgombea kule Zanzibar (ACT) alifungiwa kwa siku 5 kwa kuhamasisha wapigakura wake kwenda kupiga kura tarehe 27 Okt 2020. Mgombea wa CCM pia alisikika akitoa ujumbe huo huo, tena kwenye tepu/mkanda. ACT walipolalamika, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwa mgobea wa CCM.

Vyama viliruhusiwa kuunga mkono chama tawala lakini vikakatazwa kuunga mkono vyama vikuu vya upinzani! Haya yote yalifanyika chini ya sheria moja za nchi moja ya Tanzania.

NEC ambayo ni chombo cha kutoa haki kwa wagombea kilikuwa kinyume kabisa. Ghafla NEC walishindwa kujua kuwa katika Alfabeti, huwa inaanza A (ACT nk) halafu ndio herufi nyingine zinafuata. Wakaamua kuanza na C (CCM) kwenye karatasi ya kura! Na C nyingine (CHADEMA) ikawekwa mwisho kabisa mwa karatasi ya kura.

NEC na Msajili wa Vyama walitayarisha sheria/kanuni za kufanikisha kuharibu uchaguzi na kulazimisha vyama kutia sahini. Vyama ambavyo visingesaini, visingeruhusiwa kushiriki uchaguzi! Kanuni hizo ni pamoja na NEC kutokulazimika kutoa nakala ya matokeo vituoni kwa mawakala, kuwaapisha mawakala katika makao makuu ya majimbo tu, kutokuwapa mawakala barua ya utambulisho baada ya kuapa...

Sheria inayokataza Mawaziri na Rais kutoa ahadi/pesa kwa wananchi wakati wa kampeni haikuzingatiwa kabisa. Vyama vya upinzani vilipolalamika, havikusikilizwa mwanzo hadi mwisho.

Serikali ilkataa pesa kutoka washirika wa maendeleo na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uchaguzi huu. Serikali ilikwisha panga kile ambacho sisi hatukujua mpaka upigaji kura ulipofanyika. Katika mambo hayo ni kutokuwepo kwa waangalizi kutoka nchi washirika wa maendeleo na Umoja wa Mataifa.

Kuna mgombea wa Urais na mgombea mwenza walikuwa wanasema kuwa hata wasipopigiwa kura watashinda. Wale wanaopigia kura vyama vingine wanajisumbua tu. Baada ya uchaguzi ndio nikajua walikuwa wanamaanisha nini.

Mkurugenzi wa NEC alitumika kupigia chama tawala kampeni wazi wazi bila aibu! Kuna wakati alijibu hoja za wapinzani kwa niaba ya CCM (km kuhusu madini yetu). Angalau Kaijage alikuwa kimya. Mahera alishindwa kabisa kuwa kimya! ZEC ilishirikiana na CCM kufoji fomu ya kiapo ya Maalim Seif ili kumuengua. Kugushi ni kosa la jinai lakini yaliisha kimya kimya!

Baadhi ya maamzi haya yalifanywa na watu ambao wamesomea sheria na utoaji haki, majaji "waliobobea", wengine walitumikia nchi katika ngazi ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Sijui hili linawaambia nini Watanzania kuhusu utoaji haki katika nchi yao. Watu wenye kesi mahakamani hapa Tanzania, je wana imani yoyote na mfumo wa utoaji haki nchi hii?

Uchaguzi 2020 - Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha.

1605215596755.png

1605215663091.png
 
Wana JF,

Huu uzi ni wa kumbukumbu. Weka hapa mambo yote ya kusikitisha yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa 2020. JF ni sehemu ya kuelimishana na kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tafadhali weka hapa picha, video, maelezo, ama visa vya mambo mbalimbali ya kusikitisha uliyoyashuhudia ama kuyasikia ya KUSIKITISHA kuhusu uchaguzi wa 27 na 28 Oktoba 2020. Internet imerejeshwa sasa. Lete ma-video, picha, nk ambazo ulipiga lakini haukuweza kutuma kwa kukosa internet.

Uchaguzi 2020 - Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha.

View attachment 1625181
View attachment 1625182
Ushahidi mwingine huu hapa
IMG_20201028_084726_3~3.jpg
 
Wana JF,

Huu uzi ni wa kumbukumbu. Weka hapa mambo yote ya kusikitisha yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa 2020. JF ni sehemu ya kuelimishana na kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tafadhali weka hapa picha, video, maelezo, ama visa vya mambo mbalimbali ya kusikitisha uliyoyashuhudia ama kuyasikia ya KUSIKITISHA kuhusu uchaguzi wa 27 na 28 Oktoba 2020. Internet imerejeshwa sasa. Lete ma-video, picha, nk ambazo ulipiga lakini haukuweza kutuma kwa kukosa internet.

Uchaguzi 2020 - Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha.

View attachment 1625181
View attachment 1625182
This time around.

Mtasikitishwa sana.
 
Uchaguzi huu watanzania walikataa ushoga na kuchagua hapa kazi tu
 
Back
Top Bottom