Uzi wa vyakula tu

Hivi utajuaje unga umelainika na unatakiwa kukanda kwa muda gani?
Nipe ingredients
Unaukanda mpaka ukiunyanyua unabebeka wote kwenye kikandio usinate, kama unakandia kidish mpaka kibaki kisafi kabisa kama kimeoshwa na mkono ubaki msafi hapo ndio unakuwa umelainika.

Usiweke maji mengi sana ukawa laini utasumbua na wala usiwe mgumu sana. Kwa kg 1 mm huwa naweka vikombe viwili vya maji/maziwa ( vikombe vya chai vingi kipimo kinafanana).

Ingredients mikate haina mbwembwe ni maji, mafuta, amira na chumvi tuu. Ila kunogesha kandia maziwa, weka na vanila kidogo unaweza weka yai pia.
Vanilla inaongeza radha na harufu nzuri.
 
Kwa unga nusu naweka hamira kiasi gani na baking powder?
Maziwa ya uvuguvugu? Au ya baridi tu?
 
Kwa unga nusu naweka hamira kiasi gani na baking powder?
Maziwa ya uvuguvugu? Au ya baridi tu?
Maziwa ya uvuguvugu yakiwq yamoto sana yanaunguza hamira, hamira kile kijiko kidogo cha chai kinatosha ila baking powder sijawahi kuweka kwenye mkate/ scones . Sijajua kama huwa inawekwa ngoja wajuzi pia watatuambia. Vanilla nusu kifuniko chake.
 
Sawa asante
 
Akhsante kwa somo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…