Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Mi nazipika kwa sababu watoto wanywe chai kabla ya kwenda shule na wanazipenda
Watoto huwa wanapenda sana
Mimi tatizo hata hao watoto kwa sasa hakuna

Ila nataka nijiandae tu,miaka michache mbele nakuwa na familia nisipate shida.
Pia najifunza vitu vingi, tofauti na zamani nilikuwa napenda kujifunza vitu ninavyopenda kula tu
Sasahivi nimepunguza ubinafsi,kitu naweza nisikipende mm ila mwenzangu anakipenda.
 
Mwaga tararibu wengine hatuko insta

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Haya basi

Vipimo sijui Hukadilia tu kulingana na unga wako utakadilia
Kwenye Maziwa ya vuguvugu/maji vuguvugu weka chumvi kidogo,sukari na siagi ulolainisha,na mafuta kiasi kisha koroga ili sukar iyeyuke,kisha tia hamira vijiko vikubwa viwili vya chakula au pakti nzima ile ya jero halaf koroga funika dakika tano
Utakuta hamira imeumuka ,kisha weka unga kwa beseni uwe unamwagia huo mchanganyiko kidogo kidogo huku ukikanda unga,utakanda unga mpaka donge lishikane na kwenye beseni kusibaki kitu kinanata au mikononi,kisha lipake donge lako mafuta halaf weka kwa beseni funika na kitambaa acha dakika 45,kisha funua donge lako litakuwa limeumuka hiv👇🏼👇🏼👇🏼

Halaf litoe upepo kwa kuingiza ngu mi na sio vidole ulikande kidgo kisha paka mafuta acha liumuke tena dakika 30 ,utakuta limejaa tena kanda anza kukata viduara ya skonsi,chombo cha kubake paka mafuta au blueband kisha ziache dakika kumi umezifunika,washa oven joto weka 180 ,dakika 20 zitakuwa tayariii
Halaf zitoe paka mafuta kwa juu ya skonz zifunike dakika hata moja tu zinakuwa laini balaaa na tamuu
Ukitaka ziwe na rangi ilokoza kwa juu ya skonzi paka yai,unakoroga ya moja unapaka kwa juu rangi inakuwa bomba zaidi
Sijui umenielewaaa 😂😂😂
 

Attachments

  • 680C56DC-2270-4026-A554-F8A7DF46491B.jpeg
    680C56DC-2270-4026-A554-F8A7DF46491B.jpeg
    479.6 KB · Views: 11
Sana aisee kukanda kusukuma yeee
Mimi mzee alikuwa anapenda sana
Nikawa napika kwa ajili yake

Enzi hizo unakuta weekend wajukuu wote wanakuja
Aisee,unaweza pika chapati hata 40
Asubuhi yangu yote naua kwa kupika chapati
Natoka hapo hoii.

Sasahivi napika mara chache sana,yaani mara moja moja mno baada ya miezi kadhaa.
Kuna mama jirani anapika za kuuza,anapika vizuri halafu ni msafi,najikuta nachukua hapo.
 
Watoto huwa wanapenda sana
Mimi tatizo hata hao watoto kwa sasa hakuna

Ila nataka nijiandae tu,miaka michache mbele nakuwa na familia nisipate shida.
Pia najifunza vitu vingi, tofauti na zamani nilikuwa napenda kujifunza vitu ninavyopenda kula tu
Sasahivi nimepunguza ubinafsi,kitu naweza nisikipende mm ila mwenzangu anakipenda.
Sawa tujifunze tu ni vizuri vitu kujipikia nyumbani
 
Nzurii
Hebu elekeza hapa nami nijaribu kupika huu ni ugonjwa ujue [emoji23][emoji23][emoji23]
Mm hapo nilitumia:
Unga wa ngano 3/4
Sukari kijiko 1½ cha chakula (sio lazma )
Chumvi kijiko 1 kidogo (cha chai)
Mafuta
Maziwa uvuguvugu kikombe(cha chai) 1¼ .

Maandalizi:
  • Changanya unga, sukari, na chumvi pamoja.
  • Mimina maziwa na kidogo kidogo kwenye uga wako huku ukiukanda had ungawako uwe mlaini (itakuwa kama unanata kwenye mikono ila usijali sana)
  • Mimina kijiko 1-2 vya mafuta ya kula au kijiko kimoja cha margarine na uendelee kukanda (hapa Donge lako litakuwa kama linakatika katika hiv ila wewe endelea kukanda mpaka lishikane tena na kuwa lain.
  • Weka unga kwenye chombo chako na uufinike japo kwa dakika 15-30. Unga ukiachwa ukapumzika baada ya kuukanda unakuwa mlaini.
  • Kata madonge kwa size unayo ipenda (kwa unga 3/4 mm natoa madonge 12) na anza kusukuma moja moja lisiwe nene sana kisha pakaa mafuka kijiko kimoja (kisijae sana) kama hv 👇
    IMG_20230315_092226.jpg
    then kuna (kuna namna nyingi za kukunja ata kueleza sijui😂😂.
  • Ukimaliza zifunike kama dakika 5 then weka unga kwenye kisukumio chako anza kusukuma moja moja.
  • Weka kikaangia kwenye moto kikipata moto weka chakari yako bila mafuta ili ikauke kwanza (ikikauke sana ukiona imebadilika rangi kidogo tu kwa juu igeuze na ipake mafuta kijiko kimoja sasa) ichome mpaka hiive. Endelea hivyo hivyo kwa zote mpaka umalize
HIMARS
 
Back
Top Bottom