Mwaga tararibu wengine hatuko insta
Sent from my M2006C3LG using
JamiiForums mobile app
Haya basi
Vipimo sijui Hukadilia tu kulingana na unga wako utakadilia
Kwenye Maziwa ya vuguvugu/maji vuguvugu weka chumvi kidogo,sukari na siagi ulolainisha,na mafuta kiasi kisha koroga ili sukar iyeyuke,kisha tia hamira vijiko vikubwa viwili vya chakula au pakti nzima ile ya jero halaf koroga funika dakika tano
Utakuta hamira imeumuka ,kisha weka unga kwa beseni uwe unamwagia huo mchanganyiko kidogo kidogo huku ukikanda unga,utakanda unga mpaka donge lishikane na kwenye beseni kusibaki kitu kinanata au mikononi,kisha lipake donge lako mafuta halaf weka kwa beseni funika na kitambaa acha dakika 45,kisha funua donge lako litakuwa limeumuka hivππΌππΌππΌ
Halaf litoe upepo kwa kuingiza ngu mi na sio vidole ulikande kidgo kisha paka mafuta acha liumuke tena dakika 30 ,utakuta limejaa tena kanda anza kukata viduara ya skonsi,chombo cha kubake paka mafuta au blueband kisha ziache dakika kumi umezifunika,washa oven joto weka 180 ,dakika 20 zitakuwa tayariii
Halaf zitoe paka mafuta kwa juu ya skonz zifunike dakika hata moja tu zinakuwa laini balaaa na tamuu
Ukitaka ziwe na rangi ilokoza kwa juu ya skonzi paka yai,unakoroga ya moja unapaka kwa juu rangi inakuwa bomba zaidi
Sijui umenielewaaa πππ