Uzi wa vyakula tu

Hujasema hapo kwenye kukoroga unaanzaje,kuweka hiyo zest orange na juice orange umerukaaa
Weka butter na icing sugar kwenye bakuli koroga mpaka kiwe kitu kimoja ,kisha weka yai moja moja huku unakoroga ukimaliza utaweka orange zest koroga, utaanza kuweka unga wako kidogo kidogo kwa kutumia chekeche huku ukikoroga in between utakuwa unaweka orange juice kidogo kidogo. Ukimaliza utamimina huo mchanganyiko kwenye chombo cha kupikia ambacho ulikipaka butter na kunyunyuzia unga, ukiweka kwenye chombo usikoroge fanya kama unapiga piga kidogo chini ili ukae level kisha weka kwenye oven.NB kumbuka unga tulishachanganya na baking powder.
 
Sawa asante
 
Sawa nitafata vipimo
Kabla haujapika jaribu kusoma hapa
Utapata chochote na keki yako itatoka Nzuri
MAKOSA UNAYOFANYA KATIKA UPISHI WA CAKE

CAKE KUWEKA MASHIMO SHIMO KWA NDANI
-Umetumia mayai mengi kuliko yanayotakiwa
-Hukuchanganya vizuri mchanganyiko wako wukawa sawa

KEKI KUJAA MAFUTA
-Umetia siagi nyingi/mafuta mengi kuliko kipimo kinachotakiwa
-Umeyeyusha siagi, unatakiwa uitumie bila kuyeyusha
-Hukufuata vipimo

CAKE INANATA KAMA INAUNYEVU
-Umetumia sukari nyingi
-umetiq mayai mengi
-umetumia unga mbaya tumia unga wa cake.
-umeacha sana kuitoa kwenye tin ikaweka unyevu
-maji mengi au maziwa

KEKI HAIJAUMUKA
-Umetia baking powder kidogo/umeupiga sana mchanganyiko umeua nguvu ya bakingpoda
-Moto ulikuw mdogo
-chombo kilikua kipana sana
- umeacha sana mchanganyiko kabla hujaupika
-hukuchanganya mahitaji kama inavyotakiwa

KEKI IMEWEKA MLIMA/ IMEPASUKA JUU
-Umeupiga sana mchanganyiko wa siagi au mayai
-moto ulikua mwingi

KEKI IMEWEKA SHIMO KATIKATI
-Kufunua funua ukaingiza hewa.
-Moto mdogo
-sukari nyingi au siagi nyingi
-umechanganya sana mchanganyiko wako

KEKI IMEKUA LAINI SABA MPAKA INAMOMONYOKA
-Umetumia sukari nyingi
-umetumiq baking poda nyingi
-umechanganya vibaya
umetumia mafuta/ siagi nyingi
 
Nzuri
 

Sawa asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…