Uzi wa vyakula tu

Supu tena ya kuku ilivyo tamu

Anna niambie nimekosea wapi nilipika cake ya robo sasa nilitakiwa niweke vikombe viwili vya unga mi nikaweka kimoja
Blueband 250g
Mayai manne
Unga robo (je nilitakiwa niweke wote maana kama mafuta yamezidi hivi [emoji23][emoji23]
Hivi kaka unaweka maji au maziwa yawe ya uvuguvugu ??


 
Blueband ungeweka 200g
Unga 300

Hapo Blueband imezidi ndo maana inaonekana Ina mafuta.


Jaribu tena,

Sukari 80g
Siagi(Tumia prestige) 130g
Unga 200g
Mayai 4


Ukitaka kuweka maziwa basi weka maziwa fresh
Recipe Yake ni tofauti.


Ukitaka kuweka maji,sishauri uweke maji ya kawaida..
Instead weka vinegar.

Nb;Ukitumia vinegar basi usiweke maji au maziwa..
 
Kwa macho tu Blueband imezidi
Mafuta yako.

250g ya Blueband no nyingi sana.
Inatakiwa isiweke mafuta kama hivi
 
Sawa shukran ijumaa nitapika tena vinegar naweka kiasi gani?ukiweka vinegar na baking poda unaweka pia ?
 
Maziwa weka maziwa fresh
Ya baridi.


Recipe ya keki iliyowekwa maziwa tumia hii
2eggs
200g unga
150g sukari
Maziwa robo kikombe
Vinegar Nusu kijiko
Ladha
Baking powder kijiko Cha chai kimoja.
 
Sawa shukran ijumaa nitapika tena vinegar naweka kiasi gani?ukiweka vinegar na baking poda unaweka pia ?
Baking powder ni compulsory kwa kweli yoyote ile.
Bila baking powder hakuna keki.

Inasaidia kuumusha na mulainisha keki.


Vinegar Mimi huwa naweka mwisho kabisa,,,nikiona mchanganyiko wangu mzito sana ndo naweka.
Huwa sizingatii kiasi,,naweka hadi ntakapoona mchanganyiko upo sawa
 
Sawaaa nimekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…