Uzi wa vyakula tu

Asante umesema ndio nimefungua huu uzi niongee hiki pia, Mshana Jr nakuomba kaka yangu nyoka, mijusi sijui kenge usiwe unatuwekea humu.

Mimi binafsi huwa nakuwa inspired sana na vyakula vya humu juzi nakula nimefungua uzi nakutana na vyakula vya ajabu niliacha kula na nilipata kichefuchefu na kinyaa kwa muda mrefu sana.

Tunaomba wote tuwe tunaweka vyakula ambacho hata mwenzio akiona anajisikia vizuri wale wa kupika tukapike sio kukatishana tamaa ya kula [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sure
Mimi mara nyingi muda wa kula ndio huwa naingia humu ili nipost chakula nilichopiga picha.

Sasa ukikutana na mavitu ya ajabu, mtu mwenye kinyaa anaweza ashinde na njaa yake.
Wengine tunalisongesha tu[emoji23].
 
Sure
Mimi mara nyingi muda wa kula ndio huwa naingia humu ili nipost chakula nilichopiga picha.

Sasa ukikutana na mavitu ya ajabu, mtu mwenye kinyaa anaweza ashinde na njaa yake.
Wengine tunalisongesha tu[emoji23].
Yaani mimi nina kinyaa siwezi endelea kula, siku ametuma nyama ya nyoka sikula kabisa nikikumbuka tuu naona mate yanajaa mdomoni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Siku hizi naingia huu uzi kwa step nikistuka usiku wa manane au alfajiri ndio napitia misosi.
 
Tutoeni ushamba
Tuambieni ni nini kwanza hicho[emoji23][emoji23][emoji23]
Kinatumika kufanya nini
Ni multicooker/ pressure cooker

Inapika wali.. kwenye wali waweza pika na pilau
Maharage na ndugu zake

Nyama na mishemsho yote

Kuna siku gas ikakata shwaa
Nikapikiamo ugali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…