Okay Ma..ila sipo vizuri kwenye kuelekeza jikaze tu uelewe lol
Nimetumia mchele nusu(loweka na chumvi..inasaidia mchele kutovunjika) nyama nusu ila nlipunguza kidogo, nyanya kubwa 6 (zisage) nyanya ya pakti 1,kitunguu thomu kimoja cha size, curry powder kijiko cha kulia kimoja, pilipili manga kijiko cha chai, vitunguu maji viwili size au waeza tumia 1 kikubwa, tangawizi na chumvi kiasi na mafuta ya kupikia.
Bandika nyama kwangulia tangawizi ya kutosha eka na chumvi ikiiva weka pembeni ila hakikisha supu imebaki ya kutosha..
Kwenye sufuria nyingine kaanga kitunguu maji, kikianza wiva weka nyanya ya pakti koroga for few minutes then mimina zile nyanya za ulizosaga..koroga kidogo then utaweka viungo vilivyobaki. Binafsi viungo(thomu curry powder na pilipili manga) napenda kuweka baada ya nyanya harufu itokee vizuri ila unaeza weka baada ya vitunguu pale.
Utaacha nyanya ziive kabisa zijitenge na mafuta, mimina supu yako ya nyama..then mimina mchele uliolowekwa onja chumvi kama ndogo ongeza. Pika kidogo mimina nyama..acha uive kuwa makini usiungue nyanya ya pakti ina tabia ya kushika kwenye sufuria.
NB..kuna viungo sikutumia kwa vile sikuwa navyo na ni optional kama Bay leaves na maggy cubes kama unavyo unaweza tumia kuongeza ladha.
Hope that helps. [emoji14]