Uzi wa vyakula tu

Weekend najaribu jaribu kupika maandazi, mara ya mwisho nimekanda unga yale maandazi Mungu ndiyo anajua, yani magumu kitenesi kilaini nakosea nini mtoto mzuri
Ukiendelea kuniita mpishi hodari utashangaa siku na mie naanza kujiita hivyo πŸ€—πŸ€—

πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ we unga ulikuwa mgumu kiasi gani mpaka yawe magumu hivyo??πŸ™ˆπŸ™ˆ Next time embu jaribu kukanda unga ambao ukibonyeza unabonyea kirahisi. Alafu weka hamira ya kutosha & acha uumuke vizuri.

Hizo mbwembwe za butter mie huwa sifanya maana sipendi vitu vingi vingi. So huwa naweka Unga, Hamira, Mafuta kidogo, Chumvi kidogo na Sukari. That's it!!!!
 
Hazard CFC poleni sana πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Embu siku nyingine jaribuni kwa kuweka simple ingredients tu (Unga/Hamira/Mafuta/Sukari/Chumvi/Maji) alafu muone itakuwaje.

Mkikanda unga usiwe mgumu sana na pia muache uumuke kabisa!! Yani kama ukikanda unakuwa nusu kwenye chombo....uache uumuke mpaka ujae kwenye chombo ndio zoezi la kukaanga lianze. Na ukitaka uumuke vizuri uweke sehemu yenye joto la wastani (mf. juani, pembeni ya jiko au hata kwenye oven ila hapa inabifi uwashe kidogo ipate joto alafu uzime ndo uweke unga wako).
 
Huweki baking powder?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…