Uzi wa vyakula tu

Ugonjwa wangu ila ndo sijawahi zipatia hata sielewi nakwama wapi!

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app

Jaribu hii




menya ndizi zako vizuri toa moyo kwenye ndizi yako osha
panga majani ya ndizi kwenye sufuria yako panga ndizi zako vzr kwenye sufuria
Kuna Nazi chuja tui mara2 tui zito na tuikawaida Anza kuweka tuikawaida kwenye sufuria yenye ndizi bandika jikoni
weka chumvi kidogo Sanaa na sukari.saizi yako(kisia)
usifunike acha zichemke Hadi ziive vizuri epua

chukua sufuria Safi weka tui lako zito weka CASTAD kijiko kimoja,hiriki, ZABIBU KAVU kiasi maziwa unga vijiko 2 koroga vizuri bandika jikoni ianze kuchemka motomdogo uku unakoroga usiachie hata DK moja Hadi tui liwe zito Sanaa weka sukari kiduchu kwenye tui koroga zaidi na uepue mimina tui lilotoka jikoni kwenye ndizi zako na tikisa sufuria usikoroge tayari kwa kuliwa
 
Shukrani [emoji120] ubarikiwe sana mpendwa.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…