Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

ugali kitimoto
20190103_212046.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jinsi ya kupika bumunda
Recipe
Unga wa Ngano au ndizi kikombe kimoja
Ndizi mbivu mbili
Jani la mgomba
Mkaa

Mapishi
Koroga Unga wa Ngano au wa mahindiNa ndizi
Ukishapata hilo libonge
Lisokotee kwenye jani la mgomba lifunge vizuri kabisa
Weka mkaa juu Na chini kwa moto wa kati kwa masaa matatu


Sent using Jamii Forums mobile app

Asante mae 😘. Nilipata recipe toka kwa Idd Ninga.
Jinsi ya kupika mabumunda - JamiiForums

Sijapata ya loshoro Valentina hutengenezei laiyoni hii kitu?
 
Asante mae [emoji8]. Nilipata recipe toka kwa Idd Ninga.
Jinsi ya kupika mabumunda - JamiiForums

Sijapata ya loshoro Valentina hutengenezei laiyoni hii kitu?

Jinsi ya kupika loshoro
Ingredients
Mahindi makati yaliyokobolewa
Maziwa
Ndizi ng'ombe
Maji
Kuna maharage fulani meusi sijui yanaitwaje kiswahili

Upishi
Injika chungu uweke mahindi na maji
Acha vichemke mpaka mahindi yaanze kuiva

Weka ndizi ziendelee kuiva na mahindi

Hakikisha mahindi na ndizi vinaiva vizuri

Ipua kisha upekeche kwa mpekecho mpaka ndizi zipotelee kwenye mahindi

Acha vipoe na uweke maziwa huku unapekecha

Weka kwenye kibuyu tayari kwa kunywa
 
Back
Top Bottom