Unaweza kujionea hapa kuwa chakula ambacho mwili wako unahitaji siyo chakula ambacho hisia zako au mdomo wako au utamaduni wako uliokulia unahitaji.
Wengi wenu hapa mkiona chakula hiki mtapatwa na kinyaa lakini ni chakula kilichojaa virutubisho na ambacho ndicho mwili wako unahitaji.
Tunasema kuwa umekua mkubwa kwenye masuala ya lishe na vyakula pale ambapo utaanza kula vyakula ambavyo mwili wako unahitaji na siyo vile ambavyo unavitamani wewe labda kwa utamu wake au kutokana na utamaduni uliokulia.
Kula vyakula ambavyo mwili wako unahitaji ni suala la kujifunza na kusoma juu ya vyakula bora na mapishi yake ili uweze kuvijua.
View attachment 1870720