Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Salmon Steak.
075caa89929c01cd0020616ea3d8ab02.jpeg
cf5a1965e1c1e79a3c54bdd06dc635cf.jpeg
 
SOMA HAPA!!!!MAMBO MUHIMU KATIKA MAPISHI[emoji1427][emoji1427][emoji1427]

[emoji637] nyama au samaki Ukitia viungo( vitunguu saum, tangawizi, masala) ongeza mafuta kidogo na mtindi vjk viwili inalainika na kunoga

[emoji638] Ukikosa vanila unaweza saga Ganda la limao bichi kuleta harufu nzuri kwenye keki au chapati maji

Ukitaka kupika mboga ya karanga, saga karanga kisha tumia maziwa kukorogea karanga badala ya maji inanoga sana
[emoji639] Chapat ukiógeza kdg nazi ya unga na ukakandia maziwa chapati inakuwa zaid ya nzuri

[emoji640] Ukitaka chips au ndiz ziwe nzuri, chemsha kdg dk 5 ipua zichuje maji then weka kwenye freezer. Ukitaka kukaanga toa pasha mafuta choma usisubiri zitoke barafu, utastaajab radha yake

[emoji642] Ukiona mafuta yamekuwa mengi kwenye supu au mchuzi tumia mkate wa siles kupitisha juu kufyonza

[emoji643] Ukitaka maharage yawe na rojo zuri,baada ya kubandika tia mafuta ya kupikia yaivie pamoja

[emoji644] Ukitengeneza juice ya rosela au ubuyu unaweza weka mchaichai pale unapochemsha juice inavutia sana

Chapati ikilala ukitaka kuipasha iwe lain ichove kwenye maji baridi na kuitoa then pasha kwenye frypan bila mafuta..itakuwa kama umepika leo

[emoji645] Ukipika matembele ukiweka tangawiz na pilipili manga yanakuwa matamu balaa

[emoji647] Juice ya parachichi weka ndimu au limao utaipenda

[emoji815] Ukitaka samaki wabichi wasivurugike au kung'ang'ania wkt wa kukaanga. Wapake unga wa ngano wakolee halafu kaanga ni watamu mno

[emoji815] Ukitaka kubadili pishi la wali weka kitungú maji, saumu na iliki kdg wkt wa kuchemsha maji then yachuje halafu pika wali wako unanukia balaa

[emoji815] Kama unatumia gesi kupikia wali, jaribu tumia maji ya baridi kupikia mchele unanoga hasa

[emoji815] Ukitaka utumbo uive haraka weka limao pekee bila chumvi kwa yatke maji ya kwanza.

1.Chumvi ikizidi kwenye mchuzi menya kiazi mbatata weka ganda acha uchemke chumvi itapungua sana

2. Ukiunguza wali kata kitunguu maji nusu weka kwenye wali Funika kwa dakika tano kinasaidia kutoa harufu ya moshi

3. Tui lisipokolea kwenye maharage weka unga wa sembe tikisa acha itokote hata kama nazi ni nusu itakua kama umeweka nazi tatu

4. Maharage ukitaka yaive upesi weka kijiko cha baking powder

5. Mchuzi wa maini ukitaka uwe rost nzito au mchuzi wowote na hauna nyanya za kutosha weka kijiko kimoja cha chakula unga wa ngano ukoroge na maji kidogo then weka kwa mchuzi wacha uchemke dk 5

6. Muhogo ukiwa hauivi weka making powder kijiko kimoja

7. Nyama ikiwa ngumu au ukitaka ilainike upesi kwangulia papai bichi

8. wali ukishika, ukiungua, kabla ya kufunikia, waweza pia tumia margarine au blue band, ukipakua harufu ya kuungua haitokuwepo tena

9.carrot iwe fresh kama imesinyaa kwa fridge weka kwenye maji ya barridi nusu saa itakua kama imetoka shamba……
Screenshot_20211123-092931.jpg
Screenshot_20211123-092916.jpg
Screenshot_20211123-092905.jpg
 
Back
Top Bottom