Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

🎾MAKOSA UNAYOFANYA KATIKA UPISHI WA CAKE🎾

🎾CAKE KUWEKA MASHIMO SHIMO KWA NDANI
-Umetumia mayai mengi kuliko yanayotakiwa
-Hukuchanganya vizuri mchanganyiko wako wukawa sawa

🎾KEKI KUJAA MAFUTA
-Umetia siagi nyingi/mafuta mengi kuliko kipimo kinachotakiwa
-Umeyeyusha siagi, unatakiwa uitumie bila kuyeyusha
-Hukufuata vipimo

🎾CAKE INANATA KAMA INAUNYEVU
-Umetumia sukari nyingi
-umetiq mayai mengi
-umetumia unga mbaya tumia unga wa cake.
-umeacha sana kuitoa kwenye tin ikaweka unyevu
-maji mengi au maziwa

🎾KEKI HAIJAUMUKA
-Umetia baking powder kidogo/umeupiga sana mchanganyiko umeua nguvu ya bakingpoda
-Moto ulikuw mdogo
-chombo kilikua kipana sana
- umeacha sana mchanganyiko kabla hujaupika
-hukuchanganya mahitaji kama inavyotakiwa

🎾KEKI IMEWEKA MLIMA/ IMEPASUKA JUU
-Umeupiga sana mchanganyiko wa siagi au mayai
-moto ulikua mwingi

🎾KEKI IMEWEKA SHIMO KATIKATI
-Kufunua funua ukaingiza hewa.
-Moto mdogo
-sukari nyingi au siagi nyingi
-umechanganya sana mchanganyiko wako

🎾KEKI IMEKUA LAINI SABA MPAKA INAMOMONYOKA
-Umetumia sukari nyingi
-umetumiq baking poda nyingi
-umechanganya vibaya
umetumia mafuta/ siagi nyingi
Asante dear
 
😊
 

Attachments

  • IMG_20230510_163321_911.jpg
    IMG_20230510_163321_911.jpg
    725.8 KB · Views: 7
Kama unatumia oven set moto 160(inategemea na oven yako) chini dk45,,keki ikishapanda weka moto wa juu kwa dk 10.

Siku hizi mabaker wanapikia moto wa chini mwanzo mwisho.
Juu anaset mwisho kabisa wakati keki ishaiva ili apate tu ile rangi ya brown.
Nzuri sana ni kiasi gani hii
Hivi oven inatakiwa iwe imeshika sana moto ndio uweke au joto la kawaida tu ndio uweke cake iive
 
Kama unatumia oven set moto 160(inategemea na oven yako) chini dk45,,keki ikishapanda weka moto wa juu kwa dk 10.

Siku hizi mabaker wanapikia moto wa chini mwanzo mwisho.
Juu anaset mwisho kabisa wakati keki ishaiva ili apate tu ile rangi ya brown.
Rangi ya brown inavutia zaidii
 
Back
Top Bottom