Uzinduzi rasmi wa kampeni ya Wananchi na Katiba ‘WAKA’ kufanyika tarehe 28/8/2021 jijini Dar es Salaam

Uzinduzi rasmi wa kampeni ya Wananchi na Katiba ‘WAKA’ kufanyika tarehe 28/8/2021 jijini Dar es Salaam

UZINDUZI RASMI WA KAMPENI YA "WAKA" TAREHE 28/08/2021

WAKA Wananchi&Katiba

Dar es salaam., Tanzania
9 JUL 2021 —

Nachukua fursa hii kuwatangazia kua Uzinduzi rasmi wa Kampeni ya WAKA (Wananchi na Katiba) utafanyika tarehe 28/08/2021 ukumbi wa LAMADA HOTEL, ILALA - DAR ES SALAAM kuanzia saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 8 mchana.

Nyote mnakaribishwa kwenye kongamano hilo.

Pia nichukue fursa hii kuwafahamisha kua Jaribio la Daftari la WAKA (Wanancbi & Katiba) linaendelea katika wilaya mbalimbali za Jiji la Dar es salaam.

WAKA tunawashukuru wananchi wenzetu kwa ushirikiano.

Yahaya Omary Mpanda.

View attachment 1885141
Naomba nijumuishwe tumfurushe mama. Katiba itapatikana endapo wananchi tukiungana.
Hili jambo lisiwe la kisiasa.
Viongozi wa siasa wawaachie wananchi wajiendeshe.
 
Naomba nijumuishwe tumfurushe mama. Katiba itapatikana endapo wananchi tukiungana.
Hili jambo lisiwe la kisiasa.
Viongozi wa siasa wawaachie wananchi wajiendeshe.
Kufanya harakati za katiba mpya yenyewe ni siasa halafu unataka viongozi wa siasa waache ?
 
Mtawaka nyie mapema sana ,ukuta uko wapi wau ukawa

USSR
Mkuu kwani katiba kwenu ina shida gani?
Naona mnavyoipinga kwa nguvu zote. Yaani mpo tayari hata kuua na kuwafunga watu kisa tu wanadai katiba mpya ambao ndio mwongozo wao. Kwani mnataka muwaongoze watu kwa hisani zenu?

Mnavyokomalia kuwakataza ndio mnawafungua akili watanzania.
 
Napendekeza na tasisi nyingine zijitokeze kudai katiba mpya.
Tuelimishane kwenye vijiwe vya bodaboda,bajaji,machinga kunasiku wataelewa tu
umuhimu wa katiba mpya.
chama kimoja kinatuchagulia watu inayowataka wao na sio tunao wataka sisi.
 
Mkuu kwani katiba kwenu ina shida gani?
Naona mnavyoipinga kwa nguvu zote. Yaani mpo tayari hata kuua na kuwafunga watu kisa tu wanadai katiba mpya ambao ndio mwongozo wao. Kwani mnataka muwaongoze watu kwa hisani zenu?

Mnavyokomalia kuwakataza ndio mnawafungua akili watanzania.
Huyo anayepinga hajui hata anachopinga anafuata mkumbo tu.
 
Back
Top Bottom