Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Tanzania inasimama tena kwenye kilele cha mafanikio makubwa ya kiuchumi na kiufundi barani Afrika huku taifa likijiandaa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa mradi mkubwa wa kimkakati wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) huko Rufiji Jumamosi hii.
Kila Mtanzania mwenye uzalendo anakumbuka vizuri namna ambavyo mustakabali wa mradi huu ulivyokuwa njia panda kabla ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani na kuukuta ukiwa umefikia takriban asilimia 33 tu ya ujenzi.
Kwa maono ya mbali na dhamira ya dhati ya kuleta mapinduzi ya nishati Rais Samia alisimama kidete kuhakikisha fedha za ndani za Kitanzania tupu zinatolewa bila kukwama ili kazi isonge mbele usiku na mchana.
Matokeo ya usimamizi huo madhubuti ni kwamba mradi umekamilika kwa asilimia mia moja ukiwa ni ushahidi hai wa uwezo wetu wenyewe kama taifa kujiletea maendeleo makubwa.
Huu siyo mradi wa kawaida kwani ni uwekezaji wa kibingwa uliogharimu takriban trilioni 7.45 na una uwezo mkubwa wa kuzalisha megawati 2,115 zitakazoweka taifa kwenye usalama mkubwa wa nishati.
Bwawa hili lina uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo bilioni 33 za maji sawa na mara kumi ya uwezo wa Bwawa la Mtera jambo linalohakikisha uzalishaji endelevu wa umeme bila hofu ya ukame.
Hadi kufikia hivi karibuni JNHPP imekuwa ikichangia takriban asilimia 44.9 ya umeme wote unaoingia kwenye Gridi ya Taifa.
Hatua iliyosaidia kuondoa kabisa kero ya mgawo uliokuwa unatesa wananchi na viwanda vyetu.
Uzinduzi huo utaeleza rasmi na utaleta mapinduzi mapya ya kiuchumi kwa kutoa nishati ya kuaminika kwa ajili ya viwanda, biashara pamoja na fursa za kipekee za kilimo cha umwagiliaji na uvuvi.
Huu ni ushahidi thabiti kwamba mambo yanawezekana chini ya uongozi thabiti wa Rais Samia ambaye aliuacha mradi ukiwa asilimia 33 na kuhakikisha unakamilika kwa kishindo kikubwa.
Jumamosi hii tunaungana kusherehekea historia mpya ya nishati Tanzania huku tukithibitisha kwa vitendo kwamba kazi inaendelea na mafanikio ni ya Watanzania wote.