Chama Cha Mapinduzi Zanzibar leo tarehe 12 Septemba 2020 kinafanya mkutano wa uzinduzi wa Kampeni zake katika Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti. Mgombea wa Kiti cha Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dokta Hussein Ally Mwinyi ataeleza dhamira yake ya kuitumikia Zanzibar.
Mkutano huu utarushwa mubashara na vituo vya televisheni vya TBC, ZBC, Clouds TV, Channel 10 na ITV, pia matangazo yatarushwa live kupitia kurasa rasmi za Chama Cha Mapinduzi katika mitandao ya kijamii;
Twitter; @ccm_zanzibar @ccm_tanzania & @hpolepole
facebook; @zanzibarCCM na @tanzaniaCCM
Youtube
CCM Zanzibar &
CCM Tanzania
Instagram: @ccmtanzania
#YajayoNineemaTu
#TwendeNaMwinyi
#KuraKwaMwinyi2020
View attachment 1567266
Kikundi cha Zanzibar Big Star kikiwa jukwaani kutoa burudani kwa wanachama wa CCM na wananchi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti.