msafwa93
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 4,786
- 5,963
MADAM...Madam...Madam... ndizo kelele zilizosikika wakati Beutiful Onyinye, Wema Sepetu Madam alipokuwa akimtunza fedha nyingi dogo machachari wa Bendi ya Yamoto, Asilahi Isiyaka Dogo Aslay. Aslay akimwagiwa minoti na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu Madam.
Tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem na kuweka historia kwa Wema kuwa staa wa kwanza kumwaga fedha wakati wa uzinduzi wa bendi ya Yamoto.
MAMBO YALIVYOANZA
Awali, wakati bendi ya Yamoto ilipokuwa ikitumbuiza,ulifika wakati kiongozi wa bendi hiyo, Said Fella
alitambulisha uwepo wa Wema kwa kudai amemuwakilisha bebi wake, Nasibu Abdul Diamond hivyo apande jukwaani na kusema chochote lakini mrembo huyo akasema kilichompeleka ukumbini hapo ni uzinduzi wa Yamoto Band.
Jamani nimekuja hapa kwenye uzinduzi wa Bendi ya Yamoto na siyo kumuwakilisha Diamond, ya huku hayamuhusu kabisa sasa semeni niwaimbie wimbo,gani, alisikika Wema Sepetu na kuanza kuimba wimbo wa Niseme ambao mashabiki waliupendekeza.
AMWAGA FEDHA
Mrembo huyo asiyechuja tangu alipotwaa taji la u-miss Tanzania (2006), akiwa na wapambe wake, baada ya kuimba kidogo, alichukua pochi yake na kuanza kummwagia fedha mfululizo Dogo Aslay huku akiwa anamzunguka kwa kucheza.
ASLAY APAGAWA
Kwa fedha hizo zilizokadiriwa kuzidi milioni moja alizotunzwa Aslay, ilifika wakati dogo huyo akawa anaziangalia tu kama bubu na kupigwa butwaa huku akiishia kuzitazama bila kuimba chochote.
BAUNSA AMZUIA WEMA
Katika hali iliyowashangaza wengi, baunsa mmoja aliyekuwa akimlinda Wema alimzuia staa huyo kuendelea kutoa fedha zaidi akidai zimetosha ndipo akaacha na kushuka jukwaani.
KWA NINI ASLAY TU?
Wakati zoezi hilo likiendelea, kuna baadhi ya mashabiki waliibua minongono wakihoji kwa nini atunzwe Aslay peke yake wakati bendi hiyo ina wakali wengine watatu, Malomboso, Enock na Beka?
Mbona kama anampendelea Aslay tu wengine hawatunzi ona hela zote ameshikilia yeye tu kweli, inaonekana anamzimia sana Aslay, si bure, haikatazwi lakini, alihoji shabiki mmoja aliyekuwa akifuatilia
shoo hiyo.
MPAMBANO UNAENDELEA!
Wema ameonekana kuja juu kwa sasa kifedha, wiki iliyopita alifanya tukio kama hilo katika Ukumbi wa
Thai Village Masaki kwa kumtunza pesa ndefu mwanamuziki wa Bendi ya Skylight, Sam Mapenzi huku ikidaiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kumziba mdomo aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ambaye inadaiwa kwa sasa yuko vizuri kifedha.
MY TAKE
Mungu ametupa viumbe vyote akili yan hata wanyama wana akili,alichotutofautisha nao ni uwezo wa kufikiri,yani sisi binadamu ametupa uwezo wa kufikiri wakati viumbe wengne hajawapa.!
Sasa inapotokea binadamu anafanya mambo ya ajabu huwa najiuliza je mungu alimweka akili tu bila uwezo wa kufikiri au.??
Ina maana yupo sawa na mnyama kwa akili.??
Huyu wema sijui atakua lini.!!