Uzinduzi yamoto band: Wema aacha historia na kuwa staa wa kwanza kumwaga mihela dar live

Uzinduzi yamoto band: Wema aacha historia na kuwa staa wa kwanza kumwaga mihela dar live

msafwa93

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
4,786
Reaction score
5,963
“MADAM...Madam...Madam...” ndizo kelele zilizosikika wakati Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ alipokuwa akimtunza fedha nyingi dogo machachari wa Bendi ya Yamoto, Asilahi Isiyaka ‘Dogo Aslay’. Aslay akimwagiwa minoti na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
Tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem na kuweka historia kwa Wema kuwa staa wa kwanza ‘kumwaga’ fedha wakati wa uzinduzi wa bendi ya Yamoto.

MAMBO YALIVYOANZA
Awali, wakati bendi ya Yamoto ilipokuwa ikitumbuiza,ulifika wakati kiongozi wa bendi hiyo, Said Fella
alitambulisha uwepo wa Wema kwa kudai amemuwakilisha bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivyo apande jukwaani na kusema chochote lakini mrembo huyo akasema kilichompeleka ukumbini hapo ni uzinduzi wa Yamoto Band.

“Jamani nimekuja hapa kwenye uzinduzi wa Bendi ya Yamoto na siyo kumuwakilisha Diamond, ya huku hayamuhusu kabisa sasa semeni niwaimbie wimbo,gani,” alisikika Wema Sepetu na kuanza kuimba wimbo wa Niseme ambao mashabiki waliupendekeza.

AMWAGA FEDHA
Mrembo huyo asiyechuja tangu alipotwaa taji la u-miss Tanzania (2006), akiwa na wapambe wake, baada ya kuimba kidogo, alichukua pochi yake na kuanza kummwagia fedha mfululizo Dogo Aslay huku akiwa anamzunguka kwa kucheza.

ASLAY APAGAWA
Kwa fedha hizo zilizokadiriwa kuzidi milioni moja alizotunzwa Aslay, ilifika wakati dogo huyo akawa anaziangalia tu kama bubu na kupigwa butwaa huku akiishia kuzitazama bila kuimba chochote.

BAUNSA AMZUIA WEMA
Katika hali iliyowashangaza wengi, baunsa mmoja aliyekuwa akimlinda Wema alimzuia staa huyo kuendelea kutoa fedha zaidi akidai zimetosha ndipo akaacha na kushuka jukwaani.

KWA NINI ASLAY TU?
Wakati zoezi hilo likiendelea, kuna baadhi ya mashabiki waliibua minong’ono wakihoji kwa nini atunzwe Aslay peke yake wakati bendi hiyo ina wakali wengine watatu, Malomboso, Enock na Beka?
“Mbona kama anampendelea Aslay tu wengine hawatunzi ona hela zote ameshikilia yeye tu kweli, inaonekana anamzimia sana Aslay, si bure, haikatazwi lakini,” alihoji shabiki mmoja aliyekuwa akifuatilia
shoo hiyo.

MPAMBANO UNAENDELEA!
Wema ameonekana kuja juu kwa sasa kifedha, wiki iliyopita alifanya tukio kama hilo katika Ukumbi wa
Thai Village Masaki kwa kumtunza ‘pesa ndefu’ mwanamuziki wa Bendi ya Skylight, Sam Mapenzi huku ikidaiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kumziba mdomo aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ambaye inadaiwa kwa sasa yuko ‘vizuri’ kifedha.

MY TAKE
Mungu ametupa viumbe vyote akili yan hata wanyama wana akili,alichotutofautisha nao ni uwezo wa kufikiri,yani sisi binadamu ametupa uwezo wa kufikiri wakati viumbe wengne hajawapa.!
Sasa inapotokea binadamu anafanya mambo ya ajabu huwa najiuliza je mungu alimweka akili tu bila uwezo wa kufikiri au.??
Ina maana yupo sawa na mnyama kwa akili.??

Huyu wema sijui atakua lini.!!
 
Attachments

  • 1411548552430.jpg
    1411548552430.jpg
    43.2 KB · Views: 3,741
  • 1411548565663.jpg
    1411548565663.jpg
    35.6 KB · Views: 3,384
  • 1411548577038.jpg
    1411548577038.jpg
    45.3 KB · Views: 3,293
  • 1411548587982.jpg
    1411548587982.jpg
    42.8 KB · Views: 6,545
Halafu Madam hiyo suspender ilikua haifungi fresh hapo kwenye kifungo kiunoni imeachia flani

halafu baba harusi Petit nae si ilibid awe nyumbani na mkewe usiku huyoo Dar Live

mavazi haya huyo rafiki yake Wema na hicho kibukta kimembanaje.....

Kuhonga ndio Pesa ya Mkongo man inavyofanya kazi na Madam

anavyopenda Sifa.......
 
Du haya mama

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Huyu msichana limbukeni jamani hajifunzi tu badala ya kujiwekea vitega uchumi ana kazi ya kuwatunza watu hela.

Atakuja kuzikumbuka na hao anaowatunza pesa akija kufulia watakuja kumuangalia km mbilimbi bovu we muache tu.
 
Halafu Madam hiyo suspender ilikua haifungi fresh hapo kwenye kifungo kiunoni imeachia flani

halafu baba harusi Petit nae si ilibid awe nyumbani na mkewe usiku huyoo Dar Live

mavazi haya huyo rafiki yake Wema na hicho kibukta kimembanaje.....

Kuhonga ndio Pesa ya Mkongo man inavyofanya kazi na Madam

anavyopenda Sifa.......

Mbeba pochi hana likizo ujue...mke anapigwa na baridi yeye yuko busy na pochi ya madame
 
Mimi huo wimbo wa niseme napenda pale mwanzo yule jamaa ana base flan hivi tamu na alipoimba aslay kidogo...huko kwingine sina time ya kusikiliza...
 
Mbeba pochi hana likizo ujue...mke anapigwa na baridi yeye yuko busy na pochi ya madame

Mke mwenyewe ( Esma) Mama Kijacho inabidi mme awepo karibu..........

Muacheni tu Diamond achukie... maana akiwaza anavyofanya kazi kwa bidii

then aoe mke kazi yake kutunza majukwaani...
 
Huyu msichana limbukeni jamani hajifunzi tu badala ya kujiwekea vitega uchumi ana kazi ya kuwatunza watu hela.

Atakuja kuzikumbuka na hao anaowatunza pesa akija kufulia watakuja kumuangalia km mbilimbi bovu we muache tu.

hahaaaa mbilimbi mbovi
 
Huyu alie mroga keshakufa haponi tena,yani unakaa nyumba yakukodi hela unatupa kununua umaarufu,watu kama hawa hawakuwahi kuziona hizi pesa wakiwa watoto wamezikuta ukubwani ndio mana wanalimkuba... mwanamke nyumba yako mwanamke vitega uchumu,yeye K ndio kitega uchumi asara yake mkodombwe......
 
ni binti mdogo wa miaka 22 na ameweka historia ya kumwaga hela jukwaani nyingi kiasi kile, sijui itavunjwa lini?
 
Huyu msichana limbukeni jamani hajifunzi tu badala ya kujiwekea vitega uchumi ana kazi ya kuwatunza watu hela.

Atakuja kuzikumbuka na hao anaowatunza pesa akija kufulia watakuja kumuangalia km mbilimbi bovu we muache tu.

Inawezekana hata hata huku kutuza (siyo kutunza) pesa anaweka kitegauchumi kwa kujiweka juu kwenye magazeti na mitandao.

Wanasema spend money to make money.

Kesho akiitwa kutaka kucheza filamu anadai dau kubwa, anawaambia "mikioni si pesa, si mmeona nimetuza mtu jana".

Strategy.

But I could be wrong. And this could be totally serendipitous.
 
Angemrushia hizo pesa bibi yake kule singida angekua kafanya la maana sana teh teh
 
Angalau naniliu yake inazalisha sasa maana dai alikuwa anakula bure..... na hivi wamemwagana mkongomani taratiiiiiiiiiiiiiiibu mfuko wake tuui

Mwache atapanye atakuja kuzikumbuka baadae

Halafu Madam hiyo suspender ilikua haifungi fresh hapo kwenye kifungo kiunoni imeachia flani

halafu baba harusi Petit nae si ilibid awe nyumbani na mkewe usiku huyoo Dar Live

mavazi haya huyo rafiki yake Wema na hicho kibukta kimembanaje.....

Kuhonga ndio Pesa ya Mkongo man inavyofanya kazi na Madam

anavyopenda Sifa.......

Ingawa sijui hapo chini anajutia nin8....
 
Back
Top Bottom