kuriandlozi
New Member
- Oct 31, 2022
- 1
- 4
Naomba na mimi leo nitoe uzoefu wangu kuhusu hawa wanaojiita wataalamu tiba za asili. Nilipatwa na changamoto mwaka huu mwanzoni mtoto wangu binti wa kike yupo kidato cha tatu alipatwa na hali isiyo kawaida. Alikuwa anasoma Boarding darasani akawa analala tu na anaweza kulala masaa24 bila kuamka wala kula.
Hiyo ni baadhi tu ya mambo aliyokuwa anayafanya sitowachosha kwa mengine. Tatizo likawa kubwa ikabidi arudishwe nyumbani na mimi ikabidi niahirishe mitihani ya CPA ilikupambana na hali ya binti yangu.
Hospitali walimfanyia vipimo vya magonjwa ya kawaida ila hawakuona chochote wakashauri nimpeleke kwa psychiatrist(wataalamu wa magonjwa ya akili) ila nikapuuzia maana sikuamini kama mwanangu ana hilo tatizo.
Baadaye ofisini wakanishauri nimpeleke kwa hawa wataalamu wa asili (mimi saivi nawaita wapiga ramli tu). Basi tukashauriana na mke wangu tukaenda na binti yetu huyu mtaalamu alinipiga pesa nyingi sana akaja kusema kuwa matatizo ya binti yangu ni kutokanana na kuchezewa na watu ambao alisema ni ndugu wa mke wangu wamemroga kwaiyo amekuwa kama zezeta. Akadai pesa nyingine za kutengeneza dawa na nikampa akaniahidi ndani ya mwezi mtoto atakuwa safi.
Mwezi mmoja mbele tatizo ndio likawa baya zaidi badala ya afadhali, mtoto akawa anaamka usiku anaenda kulala nje kiwanjani au analala chooni yaani zile sehemu za ovyoovyo ndio analala uko. Nikaona huyu mtaalamu hamna kitu nikatafuta mtaalamu wa aina hiyo hiyo mwingine yeye pia alinipiga pesa za kutosha sana. Mwishoni akaja kusema mwanangu karogwa na upande wa ndugu zangu mimi (Hapo nimesha kosana na upande wa mke wangu kwa kuwatuhumu kumchezea binti yangu).
Nikavurugana na ndugu zangu tena wa damu kabisa lakini pamoja na kutoa pesa zote hizo binti yangu hakupona zaidi hali yake ikawa mbaya zaidi.
Nilitupa taulo nikaamua kwenda kwa wataalamu wa afya ya akili wakaanza kumhudumia walimpa dawa kidogo sana za kutumia mwezi tu lakini zaidi walikuwa wanamfanyia counselling na ndani ya miezi miwili tu hali ikaanza kurudi upya (Sikutoa hata senti maana alikuwa na bima ya afya).
Ushauri wangu.
Nawashauri wazazi na watanzania kwa ujumla hawa wanaojiita wataalamu wa tiba za asili tena mpaka vibali vya serikali wanavyo hawa ni makanjanja tu wamenigombanisha na ndugu zangu pande zote mbili mpaka imebidi niombe likizo ili niende nyumbani kuomba msamaha .
Nawashauri mnapopata matatizo kama haya pa kukimbilia kwanza ni kwa madaktari huku mkiendelea kumwomba Mungu wa mbinguni. Hawa wataalam wengi wanajifanya ni mashehe kumbe wapigaji tu dawa zao za mizizi hazitosaidia
Pia naishauri serikali kuacha kabisa kuwapa leseni hawa watu wanaharibu badala ya kutengeneza. Huu ndiyo uzoefu wangu nawaomba sana msiwa amini fedha niliyopigwa ilikuwa ni mtaji kabisa wa biashara lakini nimejifunza.
Nimeshatubu kanisani sitorudi kwa hawa wezi.