Uzoefu wangu wa Kutisha kwa Timu ambazo huenda Kucheza Mechi Khartoum Sudan

Kuna watu wanafurahi kumalizia nyumbani wana sahau ktk miaka minne ndani ya miaka miwili walitolewa hatua ya mzunguko CAF Championships hapo kwa Mkapa Wamakonde kutoka Msumbiji walipata droo na kuwatoa kwa goli la ugenini na Makirikiri waka wapiga tatu moja kwa Mkapa.

Sisi tunajua na haijalishi tunacheza wapi, ila makundi mwaka huu lazima, hata wakiingiza vifaru.
 
Umeshawapa sababu za kujitetea baada ya kutolewa..naona hapo wamescreen shot
 
Makamasi
 
Kweli miaka imeenda, zamani hao Wasudan walikuwa wanazihofia timu za Tanzania mno...

Wakikua kuna Yanga au Simba mbele yao, walikuwa wanajua kuna kufa au kupona...
Sasa hivi Wabongo tumewekeza chuki na roho mbaya.

Sasa hivi hata Waganda wanatunyoosha wakati walikuwa vibonde wetu.

Bora hata Wakenya wao wameamuwa kuwekeza kwenye siasa tu wajuwe moja.
 
Mbona hao walipigwa na TP Mazembe 3 bila hapo hapo Sudan, kama haujui haujui tu, km unajua unajua tu
 
Mbona st george sikusikia wamefanyiwa ayo unayoyasema, yote kwa yote boli litapigwa tena litatembezwa hasa mwenye uwezo ndio atakwenda hatua inayofata, mambo ya kutishana ayana nafasi kwa sasa wataandaliwa stahiki yao wanayostahili akuna cha msalia mtume hapo, afe kipa afe beki lazima yanga atinge makundi
 
Alafu wakapata kigoli cha penalti dk ya 85 alafu kuna kenge zinanyanyua midomo eti "thimu atari iyoooo" yaani timu hatari imepita kwa faida ya goli la ugenini? Imebutuliwa 2 kwa moja ugenini na timu legelege ya st george iliyocheza na simba hapa mechi ya kirafiki na bado ikashindwa kupata goli la mipango uwanjani ikasubilia ipewe hisani ya penalt na mwamuzi, hivi kwa hali ya kawaida kikosi cha st george na yanga ni kikosi kipi kiko bora zaidi ya kingine? Sasa kama st george kapata matokeo kwa hal hilal yanga na ubora wao ndo washindwe?
 
Hao Al hilal tunawapiga nje ndani, hii siyo Yanga ya kina Ditram Nchimbi ndio mnategemea awape ushindi.

Yanga inakwenda kuonesha Kwa vitendo nini maana ya uwekezaji na wachezaji kama Aziz Ki wanakwenda kuonesha dhahiri thamani yao.
Jipeni moyo
 
Ndugu yangu Genta.

Yanga is far better than Al Hilal technically na hizo rekodi zipo ili zivunjwe.

Najua wengi wenu Makolo mnadhani kua yanga atatoka mbele ya Al Hilal Ila kiukweli tutawa surprise.

Mimi siku zote huwa ni muumini wa 'Mpira dakika 90'.

Acha muda uamue.
 
Uzuri yanga washaandaa visingizio! Hata wao wanajua hawavuki hapo!! 🤣🤣
 
Last year yanga ilipangwa kundi gan champion league?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…