BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,527
- 3,811
Salam,
Katika maisha kuna wakati unapitia mambo magumu sana mpaka unataka kukata tamaa, na ukiwa katika hali hiyo washauri wanakuwa wengi lakini huwezi kukosa mtu mmoja atakaye kwambia "Jaribu kuangalia upande wa pili", "Nenda kwa mtaalam, sio bure wewe umerogwa."
Hali hiyo nimeipitia kipindi cha nyuma, mambo yangu yalikuwa hayaendi kabisa nimebanwa hasa. Mshauri akaja akaniambia atanipeleka Kibaha kwa mganga, kweli nilienda kwa mganga. Hiyo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza katika maisha, niliogopa sana siku hiyo lakini nikasema haina jinsi.
Mganga yule ni mmama maarufu sana pale Kibaha, baada ya kufika nikapanga foleni maana kulikuwa na watu wengi kidogo. Hatimaye zamu yangu ilifika ya kumuona mtaalamu, nilipofika akasema utaniambia shida yako au nikwambie mimi?
Nikaomba aniambie, akapandisha majini pale akaanza kufunguka aliniambia vitu vingi ambavyo vyote ni vya kweli. Nikasema hapa ndio penyewe sasa, akaniambia tatizo lako ndani ya wiki moja litakuwa limeisha. Akanipa dawa za kuoga, nyingine nilioga pale pale na nyingine nilienda kuoga nyumbani.
Ikaisha wiki hamna kitu, wiki mbili mpaka mwezi tatizo bado. Ukipiga simu kuuliza akasema watu wanatofautiana, wengine dawa hufanya kazi haraka na wengine huchelewa kwa hiyo uwe mvumilivu. Mara kadhaa pia nilikuwa naenda pale kwa ajili ya kuongezewa dozi.
Baada ya miezi miwili nikaona labda tatizo langu kashindwa na hapo ka roho kwa kupenda waganga kaliniingia, nikaanza kuzunguka sehemu mbali pamoja na kuuliza watu waganga nitawapata wapi. Nilipata waganga maeneo mbalimbali; Manzese, Magomeni, Bagamoyo, Morogoro, Tanga, Iringa na Musoma.
Nilichogundua waganga wengi sana wanakwambia mambo ya kila siku ambayo hata wewe unaweza kumwambia mtu mwingine. Mganga anasema; hapa naona pesa kwako haikai (wakati hilo ni swala la kawaida kabisa) au unapishana pishana na mke wako/mume wako, huko kazini kuna watu wanakuchukia nk.
Mganga alikuwa akiniambia hayo mambo ya kawaida nilikuwa naachana nae namwambia ntarudi kupata tiba.
Kwa kipindi chote cha mwaka na kitu, sehemu zote nilizoenda ambaye aliweza kunipa taarifa sensitive ambazo najua hizi hazijui mtu ni sehemu moja tu hapo Kibaha lakini naye hakuweza kutatua matatizo yangu.
Hivyo, binafsi naona waganga hawana uwezo wa kutatua shida za watu bali wamejawa na uongo na utapeli. Huo ndio uzoefu wangu mimi kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenda kwa waganga, kama una uzoefu tofauti share na wewe.