Uzoefu wangu wa kwenda kwa Waganga kwa Mwaka mmoja

Wengine ni imani tuu kumbuka imani ina nguvu kuliko chochote kile
Wengine ni bahati tuu
Wengine walipatia na formula zikaswihi
Mkuu kuna kitu nilitaka unisaidie,ni ishu ya ushauri,,kama utaruhusu naweza kuja inbox
 
Wengine ni imani tuu kumbuka imani ina nguvu kuliko chochote kile
Wengine ni bahati tuu
Wengine walipatia na formula zikaswihi
Inaweza kuwa hivyo ila wengi wanaofanikiwa wanakuwa wanalindwa na asili au nature yake tatizo linakuwa kuipata dawa ya kutumia na akafanikiwa kuipata, mfano Kuna waliosaidiwa na ukoo kuwekewa ulinzi wakati wa kuzaliwa au babu na bibi Sasa baada ya utoto wakaanza kuchafua miili yao wakapoteza ile asili yao ya ulinzi na bahati, maana mganga wa maisha yako ni wewe mwenyewe kwa usaidizi wa elimu ya asili yako na ukienda kinyume asili inakuadhibu ila ukishituka kukaa kwenye mstari unaanza kufanikiwa tena, mfano asili ya muafrika hairuhusu kuimba chooni Sasa mtu anaenda chooni anaimba Kila siku, au kufanya mapenzi chooni au bafuni Sasa hapo ndo asili inapokuchukia bila wewe kujua, mwingine anaongea chooni na vitu vingine vingi vinavyochafua mwili mpaka kuondoka kwenye kinga yake kiasi cha mtu kushindwa kufanikiwa na kuanza kutangatanga kwa waganga.
 
Inaweza kuwa hivyo ila wengi wanaofanikiwa wanakuwa wanalindwa na asili au nature yake tatizo linakuwa kuipata dawa ya kutumia na akafanikiwa kuipata...
Mkuu hapa naona kuna LA kujifunza,natamani ungeorodhesha,hizo mambo za asili ili iwe making kuzizingatia.kwa atakae ona inafaaa
 
Mie Kuna mmoja aliniambia kuwa mwanangu ukiwa unaenda kufanya Jambo kuwa na Imani ya kuwa utafanikiwa so nikajiongezea kwenye Ile psychic power, na Jesus alihubiria kuwa na Imani tusiwe na hofu jumlisha yule jamaa anayeitwa John Murphy Ana kitabu chake anaelezea power of our subconscious mind ilivyo na nguvu
 
Daaah niliwahi kupewa dawa ya biashara na msukuma mmoja hivi yule mzee alinitengenezea dawa "mgogo" kibuyu fulani hivi nilipiga pesa kwenye hiyo biashara tatizo nilikuwa sijaoa nilikula madem na wake za watu na bahati mbaya huo mgogo ulikuwa hauruhusu kutembeaa na wanawake wengi na wao wanajileta tuu nilikula wanawake Sana Ila niligundua mali zitokanazo na madawa zipo lakini hazidumu🤞🤞
 
................."Nilichogundua waganga wengi sana wanakwambia mambo ya kila siku ambayo hata wewe unaweza kumwambia mtu mwingine. Mganga anasema; hapa naona pesa kwako haikai (wakati hilo ni swala la kawaida kabisa) au unapishana pishana na mke wako/ mme wako, huko kazini kuna watu wanakuchukia nk"
 
Salam,

Katika maisha kuna wakati unapitia mambo magumu sana mpaka unataka kukata tamaa, na ukiwa katika hali hiyo washauri wanakuwa wengi lakini huwezi kukosa mtu mmoja atakaye kwambia "Jaribu kuangalia upande wa pili", "Nenda kwa mtaalam, sio bure wewe umerogwa."

Hali hiyo nimeipitia kipindi cha nyuma, mambo yangu yalikuwa hayaendi kabisa nimebanwa hasa. Mshauri akaja akaniambia atanipeleka Kibaha kwa mganga, kweli nilienda kwa mganga. Hiyo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza katika maisha, niliogopa sana siku hiyo lakini nikasema haina jinsi.

Mganga yule ni mmama maarufu sana pale Kibaha, baada ya kufika nikapanga foleni maana kulikuwa na watu wengi kidogo. Hatimae zam yangu ilifika ya kumuona mtaalamu, nilipofika akasema utaniambia shida yako au nikwambie mimi?

Nikaomba aniambie, akapandisha majini pale akaanza kufunguka aliniambia vitu vingi ambavyo vyote ni vya kweli. Nikasema hapa ndio penyewe sasa, akaniambia tatizo lako ndani ya wiki moja litakuwa limeisha. Akanipa dawa za kuoga, nyingine nilioga pale pale na nyingine nilienda kuoga nyumbani.

Ikaisha wiki hamna kitu, wiki mbili mpaka mwezi tatizo bado. Ukipiga simu kuuliza akasema watu wanatofautiana, wengine dawa hufanya kazi haraka na wengine huchelewa kwahyo uwe mvumilivu. Mara kadhaa pia nilikuwa naenda pale kwaajili ya kuongezewa dozi.

Baada ya miezi miwili nikaona labda tatizo langu kashindwa na hapo ka roho kwa kupenda waganga kaliniingia, nikaanza kuzunguka sehemu mbali pamoja na kuuliza watu waganga ntawapata wapi. Nilipata waganga maeneo mbali mbali; Manzese, Magomeni, Bagamoyo, Morogoro, Tanga, Iringa na Musoma.

Nilichogundua waganga wengi sana wanakwambia mambo ya kila siku ambayo hata wewe unaweza kumwambia mtu mwingine. Mganga anasema; hapa naona pesa kwako haikai (wakati hilo ni swala la kawaida kabisa) au unapishana pishana na mke wako/ mme wako, huko kazini kuna watu wanakuchukia nk.

Mganga alikuwa akiniambia hayo mambo ya kawaida nilikuwa naachana nae namwambia ntarudi kupata tiba.

Kwa kipindi chote cha mwaka na kitu, sehemu zote nilizoenda ambaye aliweza kunipa taarifa sensitive ambazo najua hizi hazijui mtu ni sehemu moja tu hapo Kibaha lakini nae hakuweza kutatua matatizo yangu.

Hivyo, binafsi naona waganga hawana uwezo wa kutatua shida za watu bali wamejawa na uongo na utapeli. Huo ndio uzoefu wangu mimi kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenda kwa waganga, kama una uzoefu tofauti share na wewe.
BABA TUPAC
 
Salam,

Katika maisha kuna wakati unapitia mambo magumu sana mpaka unataka kukata tamaa, na ukiwa katika hali hiyo washauri wanakuwa wengi lakini huwezi kukosa mtu mmoja atakaye kwambia "Jaribu kuangalia upande wa pili", "Nenda kwa mtaalam, sio bure wewe umerogwa."

Hali hiyo nimeipitia kipindi cha nyuma, mambo yangu yalikuwa hayaendi kabisa nimebanwa hasa. Mshauri akaja akaniambia atanipeleka Kibaha kwa mganga, kweli nilienda kwa mganga. Hiyo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza katika maisha, niliogopa sana siku hiyo lakini nikasema haina jinsi.

Mganga yule ni mmama maarufu sana pale Kibaha, baada ya kufika nikapanga foleni maana kulikuwa na watu wengi kidogo. Hatimaye zamu yangu ilifika ya kumuona mtaalamu, nilipofika akasema utaniambia shida yako au nikwambie mimi?

Nikaomba aniambie, akapandisha majini pale akaanza kufunguka aliniambia vitu vingi ambavyo vyote ni vya kweli. Nikasema hapa ndio penyewe sasa, akaniambia tatizo lako ndani ya wiki moja litakuwa limeisha. Akanipa dawa za kuoga, nyingine nilioga pale pale na nyingine nilienda kuoga nyumbani.

Ikaisha wiki hamna kitu, wiki mbili mpaka mwezi tatizo bado. Ukipiga simu kuuliza akasema watu wanatofautiana, wengine dawa hufanya kazi haraka na wengine huchelewa kwahyo uwe mvumilivu. Mara kadhaa pia nilikuwa naenda pale kwaajili ya kuongezewa dozi.

Baada ya miezi miwili nikaona labda tatizo langu kashindwa na hapo ka roho kwa kupenda waganga kaliniingia, nikaanza kuzunguka sehemu mbali pamoja na kuuliza watu waganga ntawapata wapi. Nilipata waganga maeneo mbali mbali; Manzese, Magomeni, Bagamoyo, Morogoro, Tanga, Iringa na Musoma.

Nilichogundua waganga wengi sana wanakwambia mambo ya kila siku ambayo hata wewe unaweza kumwambia mtu mwingine. Mganga anasema; hapa naona pesa kwako haikai (wakati hilo ni swala la kawaida kabisa) au unapishana pishana na mke wako/ mme wako, huko kazini kuna watu wanakuchukia nk.

Mganga alikuwa akiniambia hayo mambo ya kawaida nilikuwa naachana nae namwambia ntarudi kupata tiba.

Kwa kipindi chote cha mwaka na kitu, sehemu zote nilizoenda ambaye aliweza kunipa taarifa sensitive ambazo najua hizi hazijui mtu ni sehemu moja tu hapo Kibaha lakini naye hakuweza kutatua matatizo yangu.

Hivyo, binafsi naona waganga hawana uwezo wa kutatua shida za watu bali wamejawa na uongo na utapeli. Huo ndio uzoefu wangu mimi kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenda kwa waganga, kama una uzoefu tofauti share na wewe.
Wapo ila ni wachache mkuu wapo unaona live kama tv siyo stori tu
 
Huko ni uhuni tu. Me nilipewa dawa ya mpenzi nikaambiwa demu mwenyewe atanitafuta tena walikuwa mademu wawili.

Wiki ya tatu hii bado nasikilizia ila sioni dalili.

Nahesabu nimepigwa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mkuu hapa naona kuna LA kujifunza,natamani ungeorodhesha,hizo mambo za asili ili iwe making kuzizingatia.kwa atakae ona inafaaa
Ni nyingi kuorodhesha inakuwa ngumu maana Kuna za ulinzi, kuzuia kukataliwa, kuvuta mafanikio yaani ukienda nazo kinyume asili inakuadhibu hata uogee chumvi unaona mambo yanazidi kuwa mabaya tumuombe mshana akipata muda atuandikie hizo kanuni, Mimi nakupa chache tu ukizitumia hata hizo zinakupa kusaidiwa na asili bila kwenda kwa mganga, ya kwanza usiimbe chooni au bafuni wakati wa kuoga na usipende kuongea sehemu hizo wewe fanya yako toka kimya ongea baada ya kutoka huko labda kwa dharula ikitokea, hapo unazuia kukataliwa na watu au mambo yako kukataliwa, ya pili usipooze maji ya baridi kwa kutumia maji ya moto Bali pooza maji ya moto kwa kutumia maji ya baridi hasa ya kuoga pia inaondoa hasi, ya tatu usifanye mapenzi chooni au bafuni pia inaondoa nguvu za ulinzi wa asili.
 
Mkuu Mshana Jr naomba uje kusema neno hapa.
 
Duuuuh balaa ilo
 
Back
Top Bottom