A
Anonymous
Guest
Ndugu admin, naomba lifikishwe hili kwenye Wizara kama siyo Idara zinazohusika tutatuliwe hii kero.
Serikali imejitutumua kusambaza Nishati ya Umeme huku kwetu Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga lakini hatufahamu huu ni umeme wa aina gani ambao ndani ya dakika 15 hukatika kwa takriban mara 8 hadi 9 utadhani kuna mtu anachezea main switch ya kusambaza umeme mitaani?
Tunaishia kuharibiwa vyombo vyetu vinavyotumia umeme mara kwa mara.
Je, nani ashikwe shati kulishughulikia hili? Na ni kwa muda gani litakuwa limeshughulikiwa, maana huku ni hoja imepokelewa ndiyo ishatoka hiyo Limekuwa ni kero ya muda mrefu isiyotatulika.
Naomba kuwasilisha.