kwa kukusaidia zaid kabla ya wadau wenye ujuzi wao hawajafika kwanza tembelea link nilioweka hapo chini
Nataka kuagiza Subaru Forester naombeni ushauri
in general bila kujali model gani Gari za subaru kwa ujumla wake ni moja kati ya brand ambazo ni roho ya ninaweza nikaifananisha na Peagout kipindi kile, ndo maana unakuta zinatumika sana kwenye rally hasa hizo imprezza na legacy, maana yake ni kuwa they have been built to last longer and zinavumilia barabara ama aina mbali mbali za uendeshaji. si unajua gari za rally zinavyokuwa abused. hata kama mtu akinunua imprezza ya kwawaida bas anaweza akabadili vitu vichache ikawa iko tayar kwa rally tofaut na gar kama toyota allteza wengi wanaiona kama sport car ila ki ukweli haiweze kuhimili mikiki ya barabara mbovu na uendeshaj mbovu kwa mda mrefu kama subaru.
SPARE PARTS.
spare expensive ila zinalast longer, nyingi kama sio zote ni genuine na hata used bado ni bora pia , Subaru hatoi gari kama Toyota kila mwez model mpya, Subaru anatumia majina model hizo za zamani anabadil vitu vidogo ndo maana unaona kuna imprezza toka 90's na had ya 2017. na bado mjini utapata spare part ya imprezza ya 90's. sina hakina kama unaweza pata spare part ya maark II box body ama corrola zile za 90's achilia mbali kuziona mjini zikitembea.
ENGINE AND FUEL CONSUMPTION:
Subaru wanatumia Engine zinazoitwa Boxer, wanadesign na kutengeneza wenyewe, ukigoogle utapata maeleo ya ubora wa Engine za boxer na kwa nini wameziita boxer, ila kwa nyongeza ni kuwa ziko flat kw ajili ya usalama, na pia Subaru zilizotengenezwa kuanzika 96 kama sijakosea zote zimekuja na AWD manaa yake bila kujali model kuanzia imprezza ya 1.5CC had SUV Forester zote ni AWD (All wheel Drive) . angalia kwa nini Subaru wanaita AWD na sio 4WD, na angalia ubora wa AWD za gar ya aina ya Subaru na nyinginezo.
contrary to what ppl believe, Gar za subaru hazili mafuta, kwa kifupi Subaru ya CC2000 ni sawa na Carina TI cc2000 kwa manaa ya unywaj mafuta, ikiwa una Subaru ya cc2000 au 1.5cc na hupat walau 8 - 10km/L bas kuna shida kwenye gar, nimesema 8 - 10km/l kwa maana inategemea stail ya uendeshaj wako na matumiz ya AC, ila uendeshaj wa kawaida wa mjin lazima upate hapo na ukiwa high way unatakiwa upate around 13-15km/L
ni hayo tu ngoja wajuvi wa mambo waje kutumwagia mengine, kwa nyongeza ni kuwa so far gar ambazo nimeziona kwa wing hapa mjini ODODmeter ikisomeka 200K+ ni Subaru na NISSAN, na hapo engine ni ileile toka zero milage,
kwa kifupi kwa subaru utakuwa na kazi ya kurudia rangi, labda service iwe sifuri ndo utaiua
nawakilisha
natumia LEGACY B4, cc2000, MT, 10L/km, commute driving