Brother nina Legacy ya 2002, manual gear shift, imeingia ikiwa na 110,000 km, na ilikotoka haikuwa kubadilishwa Gasket na ninapoandika hii msg Odometer inasoma 195,000km.. hopefully by december nitagota 200,000km. Sijawahi badili gasket achilia mbali kugusa hata Plugs. Service Yangu ni chini tu kwenye vitu vya kureplace ( Bush, na kadhalika) CV joint nimebadili once toka 2015, Shockup toka imeingia 2015 ndo nimebadili za mbele juzi september december nabadili ya nyuma maana moja imeanza kuvuja. by the way nimeweka zote used.
Nimei abuse hii gari God knows how... maana ndo gari zetu za kimaskini wakat mwingine unapata safari ya lazima kwenda huko unakoishia kuvuma upepo inabidi uipeleke hiyo hiyo maana ndo usafiri uliopo.. njia ya kupeleka ma Offroad Mkonge unaipeleka Legacy 2002 B4. na bado gari inatoboa ukirudi service yako Kurudia rangi chini kulikochubuka... nilishawah kunasa na Hardbody nikatumia 4 hours kutoka mahali ambapo nilipita na Legacy nikanasa na kutumia 30min kutoka . ndo utofaut wa AWD ya Subaru na Other Brands
Kesi za kuunguza Gasket nimeziona online huko nchi za watu, ingawa sidhani ni kwa wingi huo. hata hapa TZ garage zote nilizotembelea sijasikia kama kesi hizo ni kidonda Sugu.
I am entitled to my opinion kwa Subaru maana nina Experience nayo kubwa tu, kwangu ni Gari ya alinunua Babu hadi mjukuu atatumia.