Uzuri wa treni ya ordinary from Dar to Kigoma

Uzuri wa treni ya ordinary from Dar to Kigoma

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
awali ya yote niwapongeze Sana TRC kwa kukarabati treni zile za zamani hasa kwa upande wa mabehewa. Mimi nasafiri Sana na hizi treni zote ,yaani deluxe na ordinary.

Treni ya ordinary ambayo ndiyo ya zamani kimabehewa Mimi kwangu ni the best treni . Sababu kuu ni hizi .
1. Imekarabatiwa kukidhi ujinga wa watanzania .Mfano vitanda vya ordinary treni vimefunikwa na turubai Laini lile la sofa ..wakati Ile ya deluxe Ina kitambaa ambayo Ina madoa madoa ya uchafu ikiashiria kuwa ule uchafu hautoki nainatia kinyaa .


2. Choo Cha ordinary kwa maana ya chumba ni kikubwa na mashimo ya kulengea mzigo ni makubwa kidogo . Wakati hizi treni za kisasa vichumba vya choo ni vifinyu mno. Harufu ya choo kwa treni ya hii kisasa ni kubwa Sana kulinganisha na hii ya kisasa ingawa zote zimewekewa wahudumu wakusafisha vyoo..hii ya ordinary wanaweka hata dawa ya kuzuia harufu hii nyingine sijaona .


3. Treni ya ordinary asilimia kubwa ya wahudumu ni watu wazima kidogo si vijana . Treni ya deluxe yaani hizi za kisasa wahudumu wengi ni dotcom generation,vijana wa 2000.


4. Ukiangalia Milango na jinsi walivyokarabati hii treni inaashiria kuwa treni ya ordinary itadumu kuliko hata hii ya kisasa.


My take , tusishobokee Sana vya wazungu kumbe na sisi tunaweza kufufua vya kwetu na kushindana na vya wazungu . Hili wazo la kukarabati haya mabehewa lilikuwa ni la magufuli , kudos Mwamba .Mungu amlaze mahali pema peponi .

Soma: TRC: Treni za SGR zilisimama maeneo matatu tofauti kutokana na hitilafu ya umeme katika Gridi ya Taifa

By uvugizi, Safarini dar from Kigoma.
 
Back
Top Bottom