Uzushi unaolenga kuwarejesha gerezani viongozi wa CHADEMA

Uzushi unaolenga kuwarejesha gerezani viongozi wa CHADEMA

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari wanaJukwaa

Wakati huu kumekuwepo na uzalishaji mkubwa wa uzushi unaoelekezwa zaidi kwenye chama tishio cha upinzani Tanzania , yaani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Na uzushi wenyewe ni wa kesi kubwakubwa za kijinai ikiwemo hilo linaloendelea mitandaoni sasa kuhusiana na uchomwaji wa vituo vya polisi n.k


Naomba nichukue nafasi hii kuwataka rai CHADEMA kutopuuzia madai haya kwani linaandaliwa bomu la kuwaweka gerezani viongozi tishio ndani ya chama tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani, malengo ya Serikali ya CCM ni kuhakikisha hawapati upinzani wa aina yoyote ukizangatia mpaka sasa hawana mgombea anayeuzika kwa wananchi.

Niwaase viongozi wa Chadema akiwemo mwenyekiti Mbowe , M/mwenyekiti Lissu , Katibu Mkuu Mnyika, na viongozi wengine wasaidizi kuhakikisha wanawahi mahakamani kudai uthibitisho wa tuhuma hizi nzito zinazoelekezwa kwao.

Asalam aleykum!
 
Polisi wetu wanatakiwa kujikita zaidi kwenye majukumu yao ya msingi. Haya mambo yao ya kujiingiza kwenye siasa za CCM na Chadema, hayajakaa sawa hata kidogo.
 
Naona kamata kamata imeanza tiyari...

Kina Boniface Jacob ni kama chambo tu ila walengwa wapo. Ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom