Uzushi wenye utata kuhusu diamond platnumz

Dong Jin

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2018
Posts
968
Reaction score
2,034
Kijana diamond toka alipoanza kufahamika mwaka 2009 kupitia wimbo wake wa nenda kamwambie amekuwa ni mtu wa kupanda tu bila kutetereka... licha ya kutabiliwa mabaya mengi lakini wapi....

Kuna uzushi ambao umekuwa ukienezwa kuwa kijana anatumia uchawi katika sanaa yake... sikatai inawezekana ni kweli lakini kwanini na hao wanaosema hivo na kututhibitishia kuwa ni kweli kijana ni noma katika anga hizo na wao wasitumie ili wawe maarufu km mond? Hv kuna mtu hapend kufika level za mondi?
Tukijaribu kuyaangazia mafanikio ya diamond kwa njia ambayo ni chanya tunamwona ni kijana anayejituma sana.... kila siku yeye amekuwa ni mtu wa kuachia nyimbo zinazopendwa na watu wa rika zote.... huwa tunaona hana maringo sana kwa mashabiki zake.. interviews zake hamung'unyi maneno... hana kisirani cha waziwazi na amekuwa akijituma sana kutowaangusha wale wanaomfuatilia....

Hivyo nyota ya kupendwa na watu, kipaji alicho nacho, na bidii katika kazi ndivyo vimemfikisha pale alipo na sio uchawi km anavyoongelewa....
Hii ya kupendwa na watu wengi na kujaza misururu ya wafuasi mara nyingi inakuwaga ni asili ya kiongozi yeyote yule... tunayaona haya kwa maraisi, na viongozi wengine wa serikali... kwa diamond yeye ni kiongozi wa mziki bongo na east africa kiujumla. Hivyo misurur ni kawaida yake ikiwa wengi wetu tunapenda burudani kuliko sanaa nyingine yeyote ile (ingekuwa brazil, mpira ungeshika hatamu).

Kupitia jina la diamod, nyota yake na jitihada zake katika kazi ndizo zikamfanya kuwasimika vijana wenzake na kuwaambukiza ile nyota yake na namna ya ufanyaji wake kazi... Tumeona namna wasanii wa wasafi wanavyotoa ngoma mfululizo bila hata ya kujali kuwa hii itaifunika iliyopita, bila hata ya kujali kuwa hii ni mbaya kuliko ile iliyopita (tunaita come back). Mfano mzuri hapa ni harmonize na wimbo wake wa "kwangwaru"... ingekuwa wengine wangeshindwa kurudi tena baada ya kutoa ngoma iliyosumbua mitaa, lakin ghafla akaibuka na atarudi ikamweka tena angani... (hapa simweki yule kijana wa kibiti, mbossokhan maana shughuli yake inafahamika kila wimbo). Ikumbukwe kuna wasanii waliwahi kutoa hit songs km darassa na ngoma yake ya "muziki" lakin alishindwa kurudi tena akapotea kwa muda. Aslay toka atoe ngoma yake nzuri ya "natamba" naye amekuwa ni wa kusuasua... hana tena ule uspesho km wa mwaka jana na juzi.
Ni hayo tu machache
NAWASILISHA
 
kijana anatumia uchawi katika sanaa yake... sikatai inawezekana ni kweli lakini kwanini na hao wanaosema hivo na kututhibitishia kuwa ni kweli kijana ni noma katika anga hizo na wao wasitumie ili wawe maarufu km mond? ...........sio kila m2 anapenda uchawi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu una amini kabisa kuwa ni ndumba ndiyo imemfkisha hapo alipo?
Hivi kazi ya kukata mauno wadhani ni mchezo. Jamaa anaweza piga show leo Mtwara kesho ana show nyingine Morogoro siyo kazi rahisi ingekuwa ndumba inaleta ela kirahisi wala asingekuwa anajituma hivyo.
Watanzania yani ni ngumu sana kukubari kwamba mtu anaweza kuanza chini aka fight akafika kwenye mafanikio makubwa ni lazima yaibuke maneno haya
Anauza ngada
Anapumuliwa
Anatumia ndumba
Siyo mali zake huyo
Tuulize sisi tunaojua
Na mengine maneno ya ajabu ajabu...........................
 
Tulikuwa kijiweni tunapiga mishe flani, kuna washkaji walikuwa wanaabudu sana ushirikina kwenye dili zetu. Mpaka leo wako palepale wanapiga dili zilezile, mi nilishawaacha kitambo.

Huwezi kufanikiwa kwa kufanya ndumba, bali kama unafanya kitu chochote lazima uwe unafanya vizuri sio kulipualipua tu. Discipline ya kazi ni muhimu kuliko mazingaombwe.
 
Kuwa namba moja milele haiwezekani ipo siku naye atapokeza kijiti kwa mwingine hiyo ndio nature mkuu haipingiki ipo siku watu watakuja kumuona DIMONDI kama mwijuma muumini kwa sasa,ingawa utapinga utasema walishatabiri lakini "HUO NDIO UKWELI" in WHOZU's VOICE.
 
Vijana siku hizi tuna roho mbaya zaidi ya wachawi, sometimes bora kampani yako iwe ya wazee wengi unaweza ukapiga hatua.
 
Sijaisoma yote ila nina cha kurekebisha mkuu. Ukisema kwann wengine nao wasitumie ndumba wawe kama Mond unakosea sana. Watu wana imani zao zinazowalinda, na ndumba ni kinyume na imani za dini. Walioshikilia imani zao hawajitesi na uchawi ili wawe juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani hapendi kufanikiwa?? Waroge nao tuwaone basi
 
Umeandika pumba zilizochanganywa na mashudu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga ujinga tu.. shule bado hazijafunguliwa???
 
Mi namkubali mondi sana


Ila katika safari yake ya mafanikio "kilinge" kimehusika pia utake usitake .

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna muujiza mahali pa wajibu....mchawi au freemason hana nguvu ya kumnyanyua mtu from empty set....na ndo mana wachawi au freemason huwa wanasubiri kwanza mtu apate mafanikio ndo wanakuja..ni uongo tuuu....Diamond analoga sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…