Dong Jin
JF-Expert Member
- Jun 4, 2018
- 968
- 2,034
Kijana diamond toka alipoanza kufahamika mwaka 2009 kupitia wimbo wake wa nenda kamwambie amekuwa ni mtu wa kupanda tu bila kutetereka... licha ya kutabiliwa mabaya mengi lakini wapi....
Kuna uzushi ambao umekuwa ukienezwa kuwa kijana anatumia uchawi katika sanaa yake... sikatai inawezekana ni kweli lakini kwanini na hao wanaosema hivo na kututhibitishia kuwa ni kweli kijana ni noma katika anga hizo na wao wasitumie ili wawe maarufu km mond? Hv kuna mtu hapend kufika level za mondi?
Tukijaribu kuyaangazia mafanikio ya diamond kwa njia ambayo ni chanya tunamwona ni kijana anayejituma sana.... kila siku yeye amekuwa ni mtu wa kuachia nyimbo zinazopendwa na watu wa rika zote.... huwa tunaona hana maringo sana kwa mashabiki zake.. interviews zake hamung'unyi maneno... hana kisirani cha waziwazi na amekuwa akijituma sana kutowaangusha wale wanaomfuatilia....
Hivyo nyota ya kupendwa na watu, kipaji alicho nacho, na bidii katika kazi ndivyo vimemfikisha pale alipo na sio uchawi km anavyoongelewa....
Hii ya kupendwa na watu wengi na kujaza misururu ya wafuasi mara nyingi inakuwaga ni asili ya kiongozi yeyote yule... tunayaona haya kwa maraisi, na viongozi wengine wa serikali... kwa diamond yeye ni kiongozi wa mziki bongo na east africa kiujumla. Hivyo misurur ni kawaida yake ikiwa wengi wetu tunapenda burudani kuliko sanaa nyingine yeyote ile (ingekuwa brazil, mpira ungeshika hatamu).
Kupitia jina la diamod, nyota yake na jitihada zake katika kazi ndizo zikamfanya kuwasimika vijana wenzake na kuwaambukiza ile nyota yake na namna ya ufanyaji wake kazi... Tumeona namna wasanii wa wasafi wanavyotoa ngoma mfululizo bila hata ya kujali kuwa hii itaifunika iliyopita, bila hata ya kujali kuwa hii ni mbaya kuliko ile iliyopita (tunaita come back). Mfano mzuri hapa ni harmonize na wimbo wake wa "kwangwaru"... ingekuwa wengine wangeshindwa kurudi tena baada ya kutoa ngoma iliyosumbua mitaa, lakin ghafla akaibuka na atarudi ikamweka tena angani... (hapa simweki yule kijana wa kibiti, mbossokhan maana shughuli yake inafahamika kila wimbo). Ikumbukwe kuna wasanii waliwahi kutoa hit songs km darassa na ngoma yake ya "muziki" lakin alishindwa kurudi tena akapotea kwa muda. Aslay toka atoe ngoma yake nzuri ya "natamba" naye amekuwa ni wa kusuasua... hana tena ule uspesho km wa mwaka jana na juzi.
Ni hayo tu machache
NAWASILISHA