V.A.R katika ligi kuu ya Tanzania bara

Kwani VAR zinafungwa upya kwa kila game, ama zikifungwa ndio zimefungwa.

Kama ni zinafungwa upya kila game na hizo ndio gharama zake basi ni gharama mnoooo.

Kama zikifungwa ndio mazima, basi tupige $150k mara idadi ya viwanja vinavyotumika ligi kuu
Tatizo Africa jau, unakumbuka final ya CL kati ya Experience na wale waarabu wenzao[emoji23][emoji23][emoji23] goli la mazabe limepigwa refa anaenda kucheki VAR anakuta imezima kitambo, likatokea timbwili na game ikaishia hapo, na rais wa caf alikuwepo uwanjani4. Nmm
 
Hahaa... Umenikumbusha kisanga.
 
Yanga watakuwa wa kwanza kupinga kwani wamewekeza mno kwa marefa
 
Kuna mechi moja ya simba na yanga walikuwa wanaonyesha supersport wakaweka big screen simba walipata bao la kusawazisha alifunga Mgosi lakini refa akakataa lakini hig screen ikawa inarudia tukio wachezaji wa simba wakamwambia refa aangalie marudio alipoangalia akabadili matokeo kwa siyo gharama kama tunavyoaminishwa na ni kitu kinachowezekana
 
Nakumbuka hii game, nilikuwa uwanjani..

Sio lazima tuingie migharama mikubwa, ni suala la kutumia akili kidogo tu.
 
Umejuaje kama TFF hawana hela?
kufunga VAR kiwanja kimoja ni $150k...tuna mechi nane kwa siku hivyo $1.2m...inawezekana kabisa...Vodacom,Azam,GSM,Mo.Taifa gas nk watoe hiyo pesa TFF waje kuwalipa kidogokidogo
 
Nakumbuka hii game, nilikuwa uwanjani..

Sio lazima tuingie migharama mikubwa, ni suala la kutumia akili kidogo tu.
Hata Arsenal vs Aston Villa, referee alitumia screen ya benchi la Arsenal baada ya VAR kuwa imezimwa.

Ni mstari mdogo unaotenganisha Live Coverage, VAR na Entire Production.
 
Hata mimi nimeunga mkono hoja. Yaani Azam wawe na kaskrin kadogo tu ka kukata mzizi wa fitina. Sisi tunataka waegemee kwenye penalt na offside. goal line technology hatuna shida nayo.
 
Hata mimi nimeunga mkono hoja. Yaani Azam wawe na kaskrin kadogo tu ka kukata mzizi wa fitina. Sisi tunataka waegemee kwenye penalt na offside. goal line technology hatuna shida nayo.
Na humu ndio hasa kwenye mapungufu yao.

Km offsidendio kabisaaa, game nyingi ukitizama unaona hili tatizo.
 
watao umia Zaidi ni mikia fc, yale magoli yao ya offside na penati za wanazopewa pewa ndiyo itakuwa basi tena..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…