Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
mkuyati og , ahsante sana mkuu kwa michango yako ambayo inatufunza mengi. Nina hoja zifuatazo, naomba usichoke kutupa elimu...
(A) Umeeleza kwamba ''ANTIBODIES do differ, in class, type and function. Even antibodies of the same class or type also differ depending on aina ya mdudu. Antibody test ya HIV ni specific to antibodies against HIV. ''
Nimeelewa vizuri sana mkuu, ila nina concern ya nYongeza: Kuna madai kwamba hizo 'specific' antibodies against HIV zaweza pia kuwa produced due to infections zingine kabsa mfano MARALIA. Pia kwamba MIMBA yaweza sababisha mwili ukaproduce hizo 'specific' antibodies against HIV !! JE UNALISEMEAJE HILI ??
(B) Umeeleza kwamba ''viral load ya HIV ni specific to HIV virus, haiinclude virusi ama wadudu wa aina nyingine''. Je hii inamaanisha kwamba kirusi wa HIV anaonekana physically (to be isolated) kabsa ili kupima/kupata viral load yake?? na Je ni kipimo gani kinachopima hiyo viral load?
Alafu kwa vile 'VIRAL LOAD' ni specific to HIV virus only, na haiinclude virusi ama wadudu wa aina nyingine (according to you), basi nadhani walitakiwa waiite 'HIV LOAD' ili kuwa 'specific' coz mwilini kuna virusi/wadudu wa aina mbali mbali. Mtazamo wangu.
(C) Umeeleza kwamba... ''The only scenario ambayo antibody test inakuwa sio conclusive ni pale ambapo utampima mtoto chini ya miezi 18 waliozaliwa na mama wenye maambukizi ya HIV sababu kipindi cha mimba na wakati wa unyonyeshaji antibodies hizi hupita na kufikia mfumo wa damu wa mtoto hivyo ukipima wakati huu unaweza kupata a false positive test maana antibodies ulizopima ni zile zilizotoka kwa mama ...''
HOJA: Just by common sense... mama mjamzito kutest HIV+ ni lazima/must pia na mtoto atazaliwa akiwa HIV+, maana mtoto akiwa tumboni anashea damu, oxygen, chakula n.k kutoka kwa mama. BUT mbona kuna wajawazito wanatest HIV+ na hawatumii ARVs ila wanazaa watoto HIV- ????
(D) Mkuu pia umetuelimisha kwamba... ''virus vya HIV pia hutofautiona kwa types na jinsi gani vina uwezo wa kusababisha dalili za ugonjwa haraka, ... Inategemea tu huyo anayekupa atakupa aina ngapi, ndio maana hata wawili wenye maambukizi bado tunashauri watumie kinga ili wasibadilishane virus wapya...''
SWALI: Je mpaka sasa, kuna types ngapi za huyu kirusi wa HIV? Je ni kweli kwamba hizi types za HIV hutofautiana kwa eneo na eneo? i.e. bara na bara (yaani regionally), mfano nasikia eti HIV wa Africa ni tofauti na HIV wa America or Europe, pia nasikia eti HIV type ya East Africa ni tofauti na HIV type ya West Africa. Hii ikoje mkuu
BY THE WAY, nilitegemea kwamba dunia nzima kungeenea Kirusi cha HIV aina moja tu kile kile kilichogunduliwa by Dr Luc & Gallo !!
(E) Kuna baadhi ya watu wanatest HIV+ na wanakaa bila kuugua (very healthy) kwa muda mrefu tu, i.e. huyo kirusi anakuwa harmless mwilini kwa muda wa miaka 10 au 15 ndipo mtu anaanza kuugua AIDS!
My concern now... mbona huu ni mda mrefu sana?? Hili wewe halikufanyi ufikiri tofauti (just to think out of the box) kuhusu HIV/AIDS hypothesis?
(F) Kuhusu ''denialism''.
Mimi binafsi sijawahi kusikia either HPV denialism! wala HEPATITIS B denialism! wala INFLUENZA denialism! n.k (I stand to be corrected). But nimekuwa nikisikia kuwa kuna HIV/AIDS denialism by competent/expert personnels of medical science. Why DENIALISM on HIV/AIDS, and not other many viral diseases?? Hili wewe halikufanyi ufikiri tofauti (just to think out of the box) kuhusu HIV/AIDS hypothesis?
Elimu muhimu sana hii. Usichoke kutuhabarisha mkuu.
Namshukuru pia mkuu Deception kwa kukubali uchokozi ili kushea knowledge katika suala hili.
kijana hongera upo vizuri sana kwa kujenga hoja zenye logic na kuuliza maswali.pia haupo biase.i like you!
Last edited by a moderator: