Valuation Calculator for Used Motor vehicles and CRSP List - TRA WANAKISIA BEI ZA MAGARI?

selemala

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2007
Posts
370
Reaction score
253
Hivi hizi bei za TRA za Magari mapya/yalipokua mapya wanazipata wapi? Mimi nina mashaka nazo sana!

Kwa mfano tuangalie bei zifuatazo za Toyota RAV4


Model Year CC Price
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR &#8804; 2003 1800 60,111 <- inawezekana Bei kuwa sawa toka 2000 ->2003 ???
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2004 1800 53,432
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2005 1800 51,206
RAV4 ZCA 3-DOOR 2000 1800 50,379
RAV4 ZCA 3-DOOR 2001 1800 57,149
RAV4 ZCA 3-DOOR 2002 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2003 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2004 1800 45,481
RAV4 ZCA 3-DOOR 2005 1800 40,932

source Tanzania Revenue Authority - Home


Fananisha bei hizo na bei ya Toyota RAV4 GX 5D Wagon 2013 - $23,300

source: Toyota Rav4 2013 | Crossover SUV


Jamaa wanakisia Ama?


Naambatanisha: Price list ya TRA ya January, 2013 (from Tanzania Revenue Authority - Home)


Halafu kuna Models nyingi za magari hazijawekwa, Je TRA wanatumia njia ipi kupata hesabu za kodi kwa models ambazo hazipo kwenye orodha yao?

Naomba kuelimishwa.
 

Attachments

Mimi si mtaalam wa masuala ya kodi, lakini haiwezekani gari ya 2005, cc3100 niinunue na kuifikisha DAR kwa Sh18M, halafu niilipie kodi zinazofika 22M!!!!!!....insane!
 
TRA tunahitaji maelezo ya hizi bei zenu!!!

Kwenye price list yenu.

1. Hakuna model zote za magari kwa miaka husika.
kwa mfano.

Model Year CC Price
CHEVROLET CRUZE - HR52S 2004 1300 XXXXX? --> na gari hizi zipo, mtaani. Walifanya vipi kujua kodi yake?

2. Inawezekana vipi, model ya gari kuwa bei moja kwa miaka minne (4)/zaidi mfululuzo?

kwa mfano.

Model Year CC Price
RAV 4 - 3 DOOR &#8805; 2005 2400 39,482
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR &#8804; 2003 1800 60,111


Napenda kuamini hamjaamua kwa makusudi KUWAIBIA WALIOAMUA KULIPA KODI KWA KUCHAKACHUA BEI ILI TU MPATE "FIGURE" MNAZOZITAKA NINYI.


Noamba kuelimishwa.
 
Mimi si mtaalam wa masuala ya kodi, lakini haiwezekani gari ya 2005, cc3100 niinunue na kuifikisha DAR kwa Sh18M, halafu niilipie kodi zinazofika 22M!!!!!!....insane!
mkuu!!manunu 18. kodi 22m!!!hii 22 ni excluding manunuzi!!!
 

Mkuu selemala, huu uzi ni wa muhimu mno, kama unaweza tafadhali badili title ya hii thread iwe kama kwenye red kisha tuwaombe mods waiweke sticky, TRA wamo wengi humu, najua hawatajibu officially lakini ujumbe utakuwa umefika!
 
Last edited by a moderator:
Kwepa kodi kila inapobidi ili uendane na sera ya maisha bora ...... Vinginevyo ukijifanya mzalendo sana itakula kwako!!! (Nasema haya nikiwa na machungu moyoni, kwani uzalendo unagharimu)

Mkuu mimi mwiba wao ulishanichoma sku hiyo mwanaume jasho lilishuka uvumilivu ukanishinda nikawaporomoshea matusi, lakini mwisho wa siku mimi ndiyo nikawa nimeliwa, WALINIOA! Toka sku hiyo mi kila inapobidi nakwepa kodi mara mwanya utokeapo!
 
Maujanja ya kukwepa kodi huwa mnafanyaje?

Kuhusu baadhi ya aina nyingi za magari kutokuwemo kwenye price list nadhani hapo maofisa wa TRA ndipo wanapomalizia hasira zao. Hiyo valuation list imewazibia sana ulaji maana ni kitu&#12288;kiko transparent, kama unajua ku-calculate haina ubabaishaji! Tatizo ni hizo aina za magari ambazo haziko kwenye list hapo lazima ni kutunishiana misuli kama ilivyokuwa enzi zile! Unawapa invoice uliyonunulia gari wanaikataa bei uliyonunulia wanabambikiza ya kwao, ukitaka nafuu inabidi hadi muongee! Tatizo ukikutana na ofisa mshenzi anaweza kukubambikizia bei kubwa sana kiasi kwamba hata mkiongea inakula kwako tu na ukileta ukali hapo ndiyo huwawezi kabisa! To make the story short gari ambalo haliko kwenye List yao silitamani wala silinunui maana kufanya hivyo nikujiweka mwenyewe kwenye mdomo wa simba!
 
Mbona TRA hawaji kujibu kama vile hawana afisa mahusiano jamani, kuweni wawazi kwa wateja wenu kwani kuelimishana kwa wastaarabu ni kawaida, mnatuumiza mno nyie TRA mnakuwa hamna huruma na ndugu zenu maskini kisa mmepewa kamshahara kazuri kuliko Dr Ulimboka uuuuffssss....
 
Hao jamaa walivyobize kukusanya mihela sijui kama hata huwa wanamuda kupita humu, maana wanajijua kuwa hawasemwi vizuri kama ilivyo kwa matrafiki.
 
Watanzamia sio kwamba hawapendi kulipa kodi, bali kodi yenyewe hailipiki. TRA ni kama miungu watu !wanachopanga wao hawazingatii hata hali halisi ya mtanzania, Hivi hujawahi jiuliza kwanini mwalimu akiwa mnoko shuleni .somo lake ndo watu wanafeli sana.
 
Tena nimeona bango lao humu ni wateja wetu, halafu wanajifanya hawaoni uzi huu!! poor customer care!
 
Hivi hakuna Tax court au independent body unayoweza kuweka malalamiko/mashtaka yako juu ya hawa TRA?
 
Jamani mimi mahesabu siyawezi vizuri hiyo calculator hata siajielewa vizuri,naomba mnisaisidie kunielekeza,mfano nikiagiza gari kuja dar, ipsum picnic ya 2004 cc 2000 kwa CIF 3000 $-yaan $2000 kununua gari na $1000 kusafirisha+insurance (kama 4.8m tzs) ntalipa sh ngapi kulitoa gari bandarini?na je TRA wanatumia bei hiyo nliyonunulia($2000) au ($3000) kufanya calculations zao au wana bei maalum kwa gari la aina hiyo nliyotaja hapo juu?
 





Ntajaribu kujibu swali lako kwa kutumia data zifuatazo - ulizozitaja.

MOdel: Toyota Ipsum Picnic
Year: 2004
Capacity: cc 2000
CIF: 3000$ ($2000 FOB $1000 kusafirisha +insurance (kama 4.8m tzs)

Kutoka kwenye Price List ya TRA version 15 (na baada ya ku-google kidogo) gari ulilotaja linafanana
na:

MOdel: Toyota IPSUM ACM 21/26
Year: 2004
Capacity: cc 2362
Price when new (Hapa ndio kwenye ugomvi, kwasababu naamini bei nyingi wamezichakachua!!): 25,014$


Maswali:

1.Ntalipa sh ngapi kulitoa gari bandarini?

TRA wanatumia bei ya gari likiwa jipya, nakufanya mahesabu ya uchakavu ili kujua thamani ya gari kwa sasa.
kwa kutumia Calculator ya TRA, Thamani ya gari hilo ( Toyota IPSUM ACM21/26 - 2004 ) ni: 3,700$

Kodi ya Jumla ni: 2,303$

Naamini kuna gharama nyingine za bandarini - naomba wadau wanazijua watusaidie.

2.Je TRA wanatumia bei hiyo nliyonunulia($2000) au ($3000) kufanya calculations zao
au wana bei maalum kwa gari la aina hiyo nliyotaja hapo juu?

TRA watatumia bei ya chini kabisa ( a minimum of) ya 3,700$ kufanya hesabu za kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…