Ntajaribu kujibu swali lako kwa kutumia data zifuatazo - ulizozitaja.
MOdel: Toyota Ipsum Picnic
Year: 2004
Capacity: cc 2000
CIF: 3000$ ($2000 FOB $1000 kusafirisha +insurance (kama 4.8m tzs)
Kutoka kwenye Price List ya TRA version 15 (na baada ya ku-google kidogo) gari ulilotaja linafanana
na:
MOdel: Toyota IPSUM ACM 21/26
Year: 2004
Capacity: cc 2362
Price when new (Hapa ndio kwenye ugomvi, kwasababu naamini bei nyingi wamezichakachua!!): 25,014$
Maswali:
1.Ntalipa sh ngapi kulitoa gari bandarini?
TRA wanatumia bei ya gari likiwa jipya, nakufanya mahesabu ya uchakavu ili kujua thamani ya gari kwa sasa.
kwa kutumia Calculator ya TRA, Thamani ya gari hilo ( Toyota IPSUM ACM21/26 - 2004 ) ni: 3,700$
Kodi ya Jumla ni: 2,303$
Naamini kuna gharama nyingine za bandarini - naomba wadau wanazijua watusaidie.
2.Je TRA wanatumia bei hiyo nliyonunulia($2000) au ($3000) kufanya calculations zao
au wana bei maalum kwa gari la aina hiyo nliyotaja hapo juu?
TRA watatumia bei ya chini kabisa ( a minimum of) ya 3,700$ kufanya hesabu za kodi.
TRA wana sababu za msingi kuweka valuation na hizo ni minimum price ikitokea CIF ya invoice yako iko
chini ya bei yao. Let say mtu mkoko wake wa zaman i for free na gharama yako ikawa ni freight na Insurance
then kwa TRA kupata thamani ya kukutoza kodi lazima wawe na estimate au valuation ya gari husika.
IPSUM 2004.
Kwa mujibu wa TRA Value ya gari hiyo ikiwa mpya kabisa ni US$ 25,014 (Retail Prece) ambapo assumption ni kuwa
bei ina Profit Margin 25%, Import Duty 25% Excise Duty 5% na VAT 18%.
Vyote Hivyo utaviondoa, na mathematically utapata US$ 12,920
Kwa gari ya mwaka 2004, ie umri zaidi ya miaka 9 lakini chini ya miaka 10 linachukuliwa kupungua thamani
kwa 70%. Kwa hiyo itakuwa imebaki na thamani ya 30%
kwa hiyo itakuwa na thamani ya US$ 3,876 (Custom Value - CV)
KODI
Import Duty (ID) 25% of CV US$ 969
Excise Duty 5% of (CV+ID) 242
VAT 18% of (CV+ID+ ED) 916
Total Tax and Duty 2,217
Exchange Rate itakuwa ya siku unayolipia/Assessiwa
Andaa not less tha TZS 500,000 kwa ajili ya clearing agent,
Port Charge, Documentation fee, Fire etc
Mdau