Valuation Calculator for Used Motor vehicles and CRSP List - TRA WANAKISIA BEI ZA MAGARI?

Valuation Calculator for Used Motor vehicles and CRSP List - TRA WANAKISIA BEI ZA MAGARI?

Kwa mujibu wa kalkuleta ya TRA kodi kwa ujumla utatakiwa kulipa TRA $ 2054 ambayo roughly ni kama TZS 3,429,841/- (assumption $1=TZS 1,670/-)..registration ni 270,000/-,shipping line ni 136,000/-,Port Charge ni 300,000/-,Agent Fee ni 200,000/- na plate number ni 38,000/- jumla kuu ni kama TZS 4,373,941/-

shukrani boss hapo nimekusoma vizuri saaaana mkuu.....
 
Jamani na mimi naomba msaada nimeagiza kagari kangu cc1490 ya mwaka 2003 kwa usd 2000 cif gari ndio ipo njiani je Nitalipia kodi sh ngapi?
 
hii ni bila ya hiyo CIF hapo juu?

nisaidie na mimi

Alteza ya kawaida
2001
cc 1900
F.O.B 2000 $

itacost kiasi gani?
 
Ntajaribu kujibu swali lako kwa kutumia data zifuatazo - ulizozitaja.

MOdel: Toyota Ipsum Picnic
Year: 2004
Capacity: cc 2000
CIF: 3000$ ($2000 FOB $1000 kusafirisha +insurance (kama 4.8m tzs)

Kutoka kwenye Price List ya TRA version 15 (na baada ya ku-google kidogo) gari ulilotaja linafanana
na:

MOdel: Toyota IPSUM ACM 21/26
Year: 2004
Capacity: cc 2362
Price when new (Hapa ndio kwenye ugomvi, kwasababu naamini bei nyingi wamezichakachua!!): 25,014$


Maswali:

1.Ntalipa sh ngapi kulitoa gari bandarini?

TRA wanatumia bei ya gari likiwa jipya, nakufanya mahesabu ya uchakavu ili kujua thamani ya gari kwa sasa.
kwa kutumia Calculator ya TRA, Thamani ya gari hilo ( Toyota IPSUM ACM21/26 - 2004 ) ni: 3,700$

Kodi ya Jumla ni: 2,303$

Naamini kuna gharama nyingine za bandarini - naomba wadau wanazijua watusaidie.

2.Je TRA wanatumia bei hiyo nliyonunulia($2000) au ($3000) kufanya calculations zao
au wana bei maalum kwa gari la aina hiyo nliyotaja hapo juu?

TRA watatumia bei ya chini kabisa ( a minimum of) ya 3,700$ kufanya hesabu za kodi.

asante mdau
 
hiyo sheet yao ya excel ni very open its a matter of plug and play.
wasiwasi wangu kama wengine walivyoweka humu ni jinsi wanavyoweka hizo price za hayo magari. Kuna mengi sana ni changa la eyes. Na kama list ipo kwa nini wakatae kuitumia wao wenyewe?
Nadhani ifike mahali tuanze kupelekana mahakamani ili watu wawajibike. U can not preach A and expect to live B. What's the exception?
Wizi tu. Sioni kama kuna mashiko sana kuwa na mkeka halafu hawautumii wao wenyewe wanakurupuka kufanya kivyao vyao. Ila pia nahisi watu wengi hawajui kama hii mikeka ipo ndo maana wanabambikiwa sana makodi yasiyokuwepo.
Yana mwisho haya yote lakini
 
TRA hawasomeki kiukweli. Calc zao haziendani na uharisia hata uduchu. Bora kununua gari iliyokwama kama hela yako niya kupima
 
ndugu zangu nataka kuagiza range rover 4.6 ya February 2000 FOB £2,995 ni kiasi kama tshs
6,901,200/=ushuru itakuwa bei gani!samahani kwa usumbufu wadau.ASANTENI.
 
Wha about Subaru Forester ya mwaka 2000 wakuu,inaweza gharimu ngapi kimahesabu ya kodi za Tra
 
Hivi hizi bei za TRA za Magari mapya/yalipokua mapya wanazipata wapi? Mimi nina mashaka nazo sana!

Kwa mfano tuangalie bei zifuatazo za Toyota RAV4


Model Year CC Price
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR &#8804; 2003 1800 60,111 <- inawezekana Bei kuwa sawa toka 2000 ->2003 ???
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2004 1800 53,432
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2005 1800 51,206
RAV4 ZCA 3-DOOR 2000 1800 50,379
RAV4 ZCA 3-DOOR 2001 1800 57,149
RAV4 ZCA 3-DOOR 2002 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2003 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2004 1800 45,481
RAV4 ZCA 3-DOOR 2005 1800 40,932

source Tanzania Revenue Authority - Home


Fananisha bei hizo na bei ya Toyota RAV4 GX 5D Wagon 2013 - $23,300

source: Toyota Rav4 2013 | Crossover SUV


Jamaa wanakisia Ama?


Naambatanisha: Price list ya TRA ya January, 2013 (from Tanzania Revenue Authority - Home)


Halafu kuna Models nyingi za magari hazijawekwa, Je TRA wanatumia njia ipi kupata hesabu za kodi kwa models ambazo hazipo kwenye orodha yao?

Naomba kuelimishwa.

TRA kuna matatizo sana,wanalalamikiwa sana but hawana nia ya kijirekebisha au kutoa elimu kwa wateja wao...badala yake elimu inayotolewa ni ya kulipa kodi ila namna gani ukadiriaji wa kodi unafanyika ni wao wenyewe.
 
TRA wanahitaji maandamano, nimenunua gari kwa shilingi 11,300000 kodi wanasema 11,350,000. Calculator inaonyesha nahitaji kulipa kodi ya 4,580,000 inakuwaje jamaniiii! nifanyaje????
 
Kabla sijaendelea niseme kwa dhati TRA hawakisii bali naamini
ni research ambazo wanafanya na kwa taarifa tu kuna idara ya
research iliyo na wanataaluma wa kufa mtu kazi zao ni nyingi
ikiwepo hii ya kuestablish best estimates za bei

Umetuambia tufananishe a bei ya Toyota RAV4 GX 5D Wagon 2013 - $23,300.
Lakini hujasema hiyo $ 23,300 ni FOB, CIF or retail price ikiwa TZ
Kufananisha lazima tufananishe vitu vilivyo ktk mazingira sawa.
Kwa kuwa site uliyoweka ni ya Toyota, then hiyo bei ni ya gari mpya
ikiwa japan, na haijalipiwa freight, insurance na kodi. Bei za TRA ni Retail Prices
yaani zimejumuisha kodi zote pamoja na faida kuanzia mtengenezaji hadi retail seller.
Pia tambua bei za mitandaoni saa nyingine ni promotion tu kuvutia watu waweze kujua
na mambo mengine, so ukitaka kujua bei halisi ya Toyota model hiyo kwa nn
usiende hapo toyota tz ukapata quatation? very ease way to clear your doubt zote.

Bei kuwa sawa toka 2000 ->2003 ???
Hapa tambua madhumuni ya kodi sio tu kukusanya mapato bali ina malengo
mengine ya kuadjust consuption za watu na for public interest at large.
Pia assumption ni kuwa consumers are rational ktk consumption.
Ukiambiwa utalipa kodi sawa kati ya 2000 model na 2003 model, ww utanunua ipi?
Kati ya model hizo 2 ipi unategemea kukupa more satsfaction.

The idea behind ni ku discourage kununua magari mabove ili kulinda walaji
na mazingira pia

Kuwa na Model Zote
Kwa TRA kuweza kuwa na Model zote ni ideal situation, and won't be possible
or impacticable. Hilizopo ni gari ambazo zinanuliwa kwa sana TZ na in case kuna
ambayo haipo then hiyo ni exception na exception haikosi soln, kama ilivyo kwenye
mahakama wanapotumia maamuzi yakimahakama yaliyofanywa na watoa maamuzi hapo
kabla au yaliyotolewa maamuzi nchi nyingine zenye
mifumo sanwa nasi (precedent) ktk kuamua swala ambalo linakuwa gumu au linakosa kifungu
sahihi kulitolea ufafanuzi.

Cheers,

Twende taratibu mkuu hapo kwenye nyekundu, kwa hiyo TRA wanaestablish bei za magari katika mchakato wa kukokotoa kodi wanatumia retail price, kwa maana bei ya gari pamoja na kodi (KODI IPI) wakati kodi ndiyo wanakokotoa?
 
Kama ntakuwa nimewaelewa TRA ni kwamba hiyo gharama ni ya gari mpya yani MSRP= manufacturer suggested retail price. Hiyo sio FOB au CIF. Kwasasa wanatumia mtindo wa kushuka thamani ( depreciation). Hivyo ukiagiza toyota RAV4 ya mwaka 2005 wao wataangalia bei ya toyota RAV4 ya mwaka 2013 yani kitu kipya kabisa mtengenezaji anauza shilingi ngapi yani MSRP ni ngapi.
MSRP wanaitoa kwasababu makampuni yanayotengeneza magari hayauzi moja kwa moja kwa mteja, wanawapa ma dealer wauze sasa wewe ukienda kwa dealer na ameongeza em 10 tafuta dealer alieongeza em 7.
HOJA YAKO: ukiambiwa angalia gari inayoendana na RAV4 kama yako haiko kwenye list ingia kwenye mtandao google linakotengenezwa hilo la kwako MSRP ni ngapi? Kama ukikuta ni $23,000 angalia hiyo inaendana na gari gani vingine unaweka kama cc, mwaka nk unapata kodi
 
Baada ya kusoma huu uzi wote, nimegundua kumbe siku hizi TRA hawahitaji kujua CIF value maana wanakokotoa kwa kutumia bei ya gari ikiwa mpya (bei ambazo wanazo wao), ila wanahitaji kujua mwaka ili kujua kama ni above or below 10 yrs. Nadhani niko sahihi kama nimewaelewa wadau mliotoa comments

Mkuu CLACET (pamoja na wadau wengine) kama unafahamu custom value ya toyota noah 2004 naomba uniambie tafadhali

Ikitokea bei uliyonunulia ni kubwa kuliko iliyo kwenye list ya tra, bei uliyonunulia inatumika.
 
Mbona TRA hawaji kujibu kama vile hawana afisa mahusiano jamani, kuweni wawazi kwa wateja wenu kwani kuelimishana kwa wastaarabu ni kawaida, mnatuumiza mno nyie TRA mnakuwa hamna huruma na ndugu zenu maskini kisa mmepewa kamshahara kazuri kuliko Dr Ulimboka uuuuffssss....

Namini ni wajibu sasa wa uongozi wa JF kufanya utaratibu wa kuwaalika hawa maafsa humu pindi inapobidi maana hali ni mbaya kuna maswali mengi kwa wizara zote, polisi, TRA na taasisi nyingine.
Mkuu Invisible tafadhali anagalia unachoweza kufanya.
 
Last edited by a moderator:
TRA wanahitaji maandamano, nimenunua gari kwa shilingi 11,300000 kodi wanasema 11,350,000. Calculator inaonyesha nahitaji kulipa kodi ya 4,580,000 inakuwaje jamaniiii! nifanyaje????
Fedhuli Tafadhali tuambie ni gari gani na ni la mwaka gani?
 
Last edited by a moderator:
Kuna jamaa yangu aliwahi kuniambia maafisa wa TRA wanamiliki wao na jamaa zao yard za kuuza magari hapa TZ kwa hiyo wanachojaribu kufanya ni kupandisha sana kodi ili ku discourage watu wasiagize magari nje ili wanunue yaliyoko kwenye yard zao wapate faida,hii nchi ubinafsi utawala.
 
TRA kuna matatizo sana,wanalalamikiwa sana but hawana nia ya kijirekebisha au kutoa elimu kwa wateja wao...badala yake elimu inayotolewa ni ya kulipa kodi ila namna gani ukadiriaji wa kodi unafanyika ni wao wenyewe.

Bora wangefanya tulipie kama sasa tunavyolipia MVehicle License KWA Mpesa itapunguza ukwapuaji wao waliouzoea
 
TRA wanahitaji maandamano, nimenunua gari kwa shilingi 11,300000 kodi wanasema 11,350,000. Calculator inaonyesha nahitaji kulipa kodi ya 4,580,000 inakuwaje jamaniiii! nifanyaje????


TRA ni mzigo kwa maendeleo ya Tanzania, hiyo calculator yao haina ukweli hata kidogo, hata ukifuata vipi inavyoelekeza ukifikisha gari mchezo tofauti. Shame on them
 
Twende taratibu mkuu hapo kwenye nyekundu, kwa hiyo TRA wanaestablish bei za magari katika mchakato wa kukokotoa kodi wanatumia retail price, kwa maana bei ya gari pamoja na kodi (KODI IPI) wakati kodi ndiyo wanakokotoa?

Wauza magari mapya hapa tanzania, TOYOTA, DT Doby na wengine si wanayalipia kodi magari yao na kuweka profit magrni yao? Hivyo bei zilizowekwa ni za retai price kwa gari jipya ambalo lishalipiwa kodi na kuwekwa profit margin. Unapotoa hiyo margin na kodi zilizolipia unapata thamani ya gari likiwa jipya kabla ya kulipiwa kodi. Baada ya hapo ndo yanakuwa depreciated kufuatana na umri ili kupata thamani ya kulitoza kodi kwa wakati huu.
Hope utakuwa umenisoma
 
Back
Top Bottom