Valuation Calculator for Used Motor vehicles and CRSP List - TRA WANAKISIA BEI ZA MAGARI?


TRA wana sababu za msingi kuweka valuation na hizo ni minimum price ikitokea CIF ya invoice yako iko
chini ya bei yao. Let say mtu mkoko wake wa zaman i for free na gharama yako ikawa ni freight na Insurance
then kwa TRA kupata thamani ya kukutoza kodi lazima wawe na estimate au valuation ya gari husika.

IPSUM 2004.
Kwa mujibu wa TRA Value ya gari hiyo ikiwa mpya kabisa ni US$ 25,014 (Retail Prece) ambapo assumption ni kuwa
bei ina Profit Margin 25%, Import Duty 25% Excise Duty 5% na VAT 18%.
Vyote Hivyo utaviondoa, na mathematically utapata US$ 12,920
Kwa gari ya mwaka 2004, ie umri zaidi ya miaka 9 lakini chini ya miaka 10 linachukuliwa kupungua thamani
kwa 70%. Kwa hiyo itakuwa imebaki na thamani ya 30%
kwa hiyo itakuwa na thamani ya US$ 3,876 (Custom Value - CV)
KODI
Import Duty (ID) 25% of CV US$ 969
Excise Duty 5% of (CV+ID) 242
VAT 18% of (CV+ID+ ED) 916
Total Tax and Duty 2,217
Exchange Rate itakuwa ya siku unayolipia/Assessiwa
Andaa not less tha TZS 500,000 kwa ajili ya clearing agent,
Port Charge, Documentation fee, Fire etc

Mdau
 


Mdau, nashukuru kwa mchango mzuri.

Lakini je hizo bei kutoka TRA za magari yakiwa mapya ni sahihi?
 

Baada ya kusoma huu uzi wote, nimegundua kumbe siku hizi TRA hawahitaji kujua CIF value maana wanakokotoa kwa kutumia bei ya gari ikiwa mpya (bei ambazo wanazo wao), ila wanahitaji kujua mwaka ili kujua kama ni above or below 10 yrs. Nadhani niko sahihi kama nimewaelewa wadau mliotoa comments

Mkuu CLACET (pamoja na wadau wengine) kama unafahamu custom value ya toyota noah 2004 naomba uniambie tafadhali
 

in tanzania import taxation is an art and not science, you pay whatever the TRA officer tells you in his/her own discretion opinion, usijaribu kuagiza gari tanzania mpaka nchi itakapo ongozwa na watu wenye akili timamu, CHADEMA.
 
Ukitaka kuingiza gari Tanzania na kulipa ushuru halali kulingana na bei ya gari uliyonunua, lazima ufanye mchakato' na huu mchakato ni kati ya wafanyakazi wa TRA na clearing agent wako, una,pa hela kidogo anarekebisha otherwise gari utanunua kwa cif ya usd 3000 utailipia hata mil 8 na hakuna wa kumlalamikia
 

Kabla sijaendelea niseme kwa dhati TRA hawakisii bali naamini
ni research ambazo wanafanya na kwa taarifa tu kuna idara ya
research iliyo na wanataaluma wa kufa mtu kazi zao ni nyingi
ikiwepo hii ya kuestablish best estimates za bei

Umetuambia tufananishe a bei ya Toyota RAV4 GX 5D Wagon 2013 - $23,300.
Lakini hujasema hiyo $ 23,300 ni FOB, CIF or retail price ikiwa TZ
Kufananisha lazima tufananishe vitu vilivyo ktk mazingira sawa.
Kwa kuwa site uliyoweka ni ya Toyota, then hiyo bei ni ya gari mpya
ikiwa japan, na haijalipiwa freight, insurance na kodi. Bei za TRA ni Retail Prices
yaani zimejumuisha kodi zote pamoja na faida kuanzia mtengenezaji hadi retail seller.
Pia tambua bei za mitandaoni saa nyingine ni promotion tu kuvutia watu waweze kujua
na mambo mengine, so ukitaka kujua bei halisi ya Toyota model hiyo kwa nn
usiende hapo toyota tz ukapata quatation? very ease way to clear your doubt zote.

Bei kuwa sawa toka 2000 ->2003 ???
Hapa tambua madhumuni ya kodi sio tu kukusanya mapato bali ina malengo
mengine ya kuadjust consuption za watu na for public interest at large.
Pia assumption ni kuwa consumers are rational ktk consumption.
Ukiambiwa utalipa kodi sawa kati ya 2000 model na 2003 model, ww utanunua ipi?
Kati ya model hizo 2 ipi unategemea kukupa more satsfaction.

The idea behind ni ku discourage kununua magari mabove ili kulinda walaji
na mazingira pia

Kuwa na Model Zote
Kwa TRA kuweza kuwa na Model zote ni ideal situation, and won't be possible
or impacticable. Hilizopo ni gari ambazo zinanuliwa kwa sana TZ na in case kuna
ambayo haipo then hiyo ni exception na exception haikosi soln, kama ilivyo kwenye
mahakama wanapotumia maamuzi yakimahakama yaliyofanywa na watoa maamuzi hapo
kabla au yaliyotolewa maamuzi nchi nyingine zenye
mifumo sanwa nasi (precedent) ktk kuamua swala ambalo linakuwa gumu au linakosa kifungu
sahihi kulitolea ufafanuzi.

Cheers,
 

Hallo Mdau,
Never late than ever!!!
Cheki hiyo simple hesabu ya kodi ya Noah 2004 model, 2WD na 4WD,

Mdau
 

Attachments

Thanks CLACET, umenipa picha kamili, sasa naweza kujipanga with confidence!
 
Mimi si mtaalam wa masuala ya kodi, lakini haiwezekani gari ya 2005, cc3100 niinunue na kuifikisha DAR kwa Sh18M, halafu niilipie kodi zinazofika 22M!!!!!!....insane!

Ndugu yangu nchi hii ni TRA ni wauwaji...yani wao hata kama wakigundua wameku charge ushuru zaidi wanakulipisha tu...nchi hii imejaa dhuluma na wantumia udhaifu wa hizi kampuni za clearing ambazo na uhakika zaidi ya 80% zinaendeshwa na watu wasioenda shule na wakati mwingine wanashirikiana nazo kuibia wateja ....mimi nimelipa ushuru 2000 Range Rover HSE 4.6 milioni 12 badala ya milion 6...na kabla sijaleta nilipeleka kwa evaluator wao akasema hiyo ikija utalipa usd 4,260...lakini hawa Clearing wakijaza kwenye hiyo Ascuda++ inakuja milioni 12...na akawa anakazania ku accept eti akichelewa atafungiwa kampuni ya ni vitu vya ajabu hata mimi nilijaribu kutumia hiyo valuation calculator inakuja TZS. 6.9m
 

Nakubaliana nawe kuwa consumer ni rational na kwa maana hiyo mtu anaponunua gari na soko liko nje say Germany sidhani kama practical kutumia bei elezekezi toka...yaani si practical. Kinachotokea kwa rational consumer ni ku-opt kununua older model/series ambayo kisheria bado inaruhusiwa legal ili asave say USD 800-1000.

Labda kuhusiana na swala la mazingira tuwekana sawa kuwa si lazima sana kama unavyosuggest kuwa the latest a car is the more environmetally frendly it is.

Tuseme ukiacha unafiki na kutetea sera za ofisi katika soko la magari hali si kama TRA wanavyofikiri/dhania...ukweli wanachofanya TRA ni kuingilia mwenendo wa soko. Gari zinauzwa ktk soko huru lenye ushidani kama vitu vinginevyo mfano vya electronics. Labda nami nipate kufahamishwa kama utaratibu huu wa magari unatumika pia kwa bidhaa zingine?
 
Hivi hakuna Tax court au independent body unayoweza kuweka malalamiko/mashtaka yako juu ya hawa TRA?

Ya ipo tena very active hapo Dar ipo jengo moja na NMB iliyopo oposite na habari maelezo.ulichokiwaza na mimi nilishawaza kukifanya
 
Hallo Mdau,
Never late than ever!!!
Cheki hiyo simple hesabu ya kodi ya Noah 2004 model, 2WD na 4WD,

Mdau

Mkuu CLACET (na ye yote anayejua jamani) nikusumbue tena! hivi gari ya 2003 ina kodi ya uchakavu? nimependa model ya 2003 ila nashindwa kuelewa vizuri hiyo miaka 10 wanahesabu vipi isije ikala kwangu.
 


[TABLE="width: 390"]
[TR]
[TD="colspan: 3"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Current Retail Selling Price[/TD]
[TD] 25,012[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Depreciation[/TD]
[TD] [/TD]
[TD]80%[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Freight[/TD]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Customs value[/TD]
[TD] [/TD]
[TD] 2,584[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]FOB Value[/TD]
[TD] 2,584[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Import Duty 25%[/TD]
[TD] 646[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Excise Base for vehicle aged more than 10 years[/TD]
[TD] 646[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Excise Base[/TD]
[TD] 3,230[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Excise Duty 5%[/TD]
[TD] 161[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]VAT Base[/TD]
[TD] 4,037[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]VAT 18%[/TD]
[TD] 727[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total Taxes[/TD]
[TD] 2,180[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Total Taxes in TSHs[/TD]
[TD] 3,488,356[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Thanks kwa wote mliotoa ufafanuzi..swali ni kuwa,hivi hao TRA wanakubali malipo kwa dola,au wameweka dola katika calculators ila kwenye malipo wanataka TZS?
 
mimi nina swali langu tofauti kidogo....kuna gari nimeipata ,ipo nchini na ina namba za ubalozini(green plates),so haijalipiwa kodi....kodi inayodaiwa ni kama 1.2M,je itanigharimu bei gani kuclear kodi na kuifanyia registration ya namba za kawaida?...kwa wale ambao mshafanya kitu kama hiki naomba mnisaidie
 
Tena nimeona bango lao humu ni wateja wetu, halafu wanajifanya hawaoni uzi huu!! poor customer care!
Bango lipo na contact za kuweza jibiwa papo kwa papozipo kwa nini hamzitumii mpaka mnataka mjibiwe kupitia JF. JF siyo official web site au blog ya TRA.
Uliza hoja na kero zako kwenye contact zilizotolewa na kama hujajibiwa ipasavyo ngazi ziko nyingi mpaka zitatatuliwa. Hizo contact ziliwekwa kwa ajili ya kupunguza na kutaka kusikiliza kero za wanajamii. kulalamika sa hakusaidii.
Jaribuni kwanza mkiona hamna response nzuri basi mrudi humu JF.
 

ebana kama mtu anaingiza
Alteza Gita
2004
cc 1990
CIF USD 2290

inaweza cost sh ngapi
 
ebana kama mtu anaingiza
Alteza Gita
2004
cc 1990
CIF USD 2290

inaweza cost sh ngapi

Kwa mujibu wa kalkuleta ya TRA kodi kwa ujumla utatakiwa kulipa TRA $ 2054 ambayo roughly ni kama TZS 3,429,841/- (assumption $1=TZS 1,670/-)..registration ni 270,000/-,shipping line ni 136,000/-,Port Charge ni 300,000/-,Agent Fee ni 200,000/- na plate number ni 38,000/- jumla kuu ni kama TZS 4,373,941/-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…