wadau kwa masikitiko makubwa nasema value retension ya 6% ya kila salio baada ya makato ni shida kubwa sana
kwanza wanufaika walilazimishwa kulipa asilimia kumi na tano wakakubali bado haitoshi wamewekewa 6% kila baada ya mwaka wa fedha kweli haki iko wapi.
watu wa sheria wanajua makubaliano ya mwaka jana wakati sheria haijabalika yatabaki yale yale hayataingiliwa lakini awamu hii wakavunja makubaliano hayo na kulazimisha watu wote walipe fifteen percent.
serikali hii inajinasibu serikali ya wanyonge wanyonge gani inawajali?
je msalaba huu kuwatwisha watoto wa maskini na kuwapaka kwa mgongo wa chupa eti serikali ya wanyonge ni sentensi nzuri kweli?
Ebu tujadiliane haya tunapoelekea serikali ya chama kimoja ccm hapo octoba itatokea nini.
Ideally kama uzalishaji wa ajira kwenye private sector ungekuwa mkubwa, graduates wangekuwa absorbed na mifumo ili walipe deni.
Serikali in most cases ni muajiri wa sekta ya huduma kuliko uzalishaji (production).
Kwa lugha nyingine, ilitakiwa kuwa na "loan board" kwa innovators/inventors ambao kila mwaka wanapata mikopo ya uwekezaji ili in the course of production of consumable products za kahawa, pamba, chai, korosho, katani, nyama, ngozi, samani mwisho wa siku watu waliosoma sales/marketing, accounts, logistics, engineering, legal, et la; wanapata kazi kwenye private and public sector.
Otheriwse kuna penalties zingine nchi hii huwa haziko realistic. Mfano, ukipigwa fine kwa traffic office ambayo ni sh. 30,000 in a week time kama hujalipa, deni likakuwa 37,500. Interest ya 25% in a week time haiko realistic.
Hakuna anaebariki makosa ya barabarani, ila interest ya 25% ndani ya siku 7, sijui walioiweka walikuwa wanafikiria nini. Na ndani ya mwaka kama haijalipwa inajilimbikiza.
Calculations za malipo ya mikopo kwa wale wanaolipa ambao ni wachache kwa kuwa kazi zinazotengenezwa ni chache, iko haja kuwekeza kwenye kutafuta watu wenye DNA ya kubuni uwekezaji wa kuzalisha products zenye uhitaji mkubwa kama uniforms za wanafunzi chekechea mpaka vyuo vya kati; vitambaa, viatu na mikanda ilitakiwa karibu vyote kwenye mnyororo wa thamani vizalishwa locally.
Sasa, ilitakiwa Wizara ya elimu iwe "education content model" toka kwenye mfumo wa elimu ikiwekwa kwenye vitendo iwe na uwezo wa kuatatua mambo haya kwa picha kubwa.
Hata watunga sheria wetu toka vyama karibu vyote pale mjengoni, wengi kwenye hard issues za mambo ya kitaifa kukuza uchumi na kuleta usatawi wa jamii pana, wapo kimyaaa; ila kwenye habari "nyepesi" na kubishabishana kila mmoja anachangamka
Shalom