Vanessa auza nakala 750 za CD ya Money Mondays

Vanessa auza nakala 750 za CD ya Money Mondays

Safi sana at least kaonesha njia, sio kilasiku kulialia tu oh wasanii tunaibiwa, imagine akifanya hivyo kwa mikoa 10 tu anapata hela ya kula mwaka mzima
 
TRA wameshapiga hesabu zao mkidaiwa kodi msikimbie
uzalendo kwanza
TRA sio dubwana kama mnavyotaka watu waamini,lipeni kodi kwa mujibu wa biashara zenu copy 750 zikiuzwaa atakuwa keshaingiza na vat humo so hakuna shida tuwasapot watu wetu ili walipe kodi huku wakitabasam na kunywa kahawa ofisi za TRA!
Tujenge utamaduni wa kuchangia katika nchi yeti sio kujitishia kodi
 
Wabongo hawana utamaduni wakununua albam na si kwamba wanakosea hapana msanii wa kibongo ni kawaida kuona ndani ya album yenye nyimbo kumi ni tatu ndizo ulizozipenda nyingine unarusha(skip) au unapeleka mbele (forward)
 
750x10,000=7,500,000/=
kwa siku

biashara tamu sana hiii naomba kujuzwa wapi naanzia ili nitoe singo wakuu
Huko nje kina Kendrick lamar wanauza copy zaidi ya million 1..... Tena copy moja bei yake mara tano zaidi ya bei anayouza mdee

Kma serikali ingebana vizuri copyright laws wasanii wangekuwa matajiri sana tofauti na sahvi hta wakitoa album wananufaika wahuni wachache
 
Haiwezi kaa itokee hiyo ndo imeishia hapo akitamba sana copy buku tuu
Kwanini isitokee mkuu ilihali nna uhakika vanessa hakosi mashabiki angalau elfu 10 kila mkoa kwa ushahidi wa tour wanazofanya.... Hivi akisema kiingilio ni elfu 15 yaani 5 ya kuingia na 10 ya album unafkiri hatofikisha nakala milion 1 kwa nchi ya vijana million 30???
 
Muziki ungewekewa misingi na kulindwa kama biashara zingine tungezalisha mamilionea toka street wengi tu.

imagine auze copy laki mbili angalau.

Cd feki zipigwe vita kama vipodozi feki au vyeti feki tutengeneze ajira za bure bure kwa masela badala ya kuwa mateja na wakabaji.
Si rahisi mkuu, imagine kuna rafiki yako maybe amenunua cd moja, wewe unaenda unamuazima unairip kwenye pc unaingiza nybo kwenye cm mchezo umeisha. Piracy ya kazi za Sanaa bado ni kikwazo kikubwa sana kwa mafanikio ya wasanii wetu hapa nchini.
 
albamu ya Ugali au A.K.A Mimi hazikufika platinum kweli??
 
Wenzake wiki ya kwanza wanagonga platinum RIAA Certfied yeye anafurahi copies 750?
Ndo kaanza.... Hujaona kuwa ni mafanikio makubwa?

Unatakaa aanze na kuuza nakala milioni na zaidi?

Tujitahidi kupeana moyo jamani why uvunje moyo mtu? Yaani kwa maoni yako we umeona si mafanikio hayo... Tumetofautiana sana hapa Duniani..

Nadhani next time utawapa moyo wasanii wetu na majirani zetu wanapoanzisha miradi mbali mbali.

For me, big up to her.
 
Back
Top Bottom