Vanilla ni fursa Njombe?

Vanilla ni fursa Njombe?

card78

Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
49
Reaction score
48
Wadau poleni na majukumu

Baada ya kipindi kirefu toka rafiki yangu anipe story juu ya zao la vanilla huko kwao Kagera na jinsi linalindwa haswa wakati wa kuvuna nilipata shauku ya kujua zaidi lakin kutokana na majukumu mengine sikuweza kufuatilia sana.
Ila kwa muda wa miezi mitatu sasa nimekuwa nikisikia matangazo kwenye Tv kuhusu Vanilla village huko Njombe na kinachonivutia na kuniogopesha pia ni juu ya bei 1kg/1M yaan hiyo hela kwa 1kg inaniogopesha sana kwan kwa maelezo ya awali niliambiwa kulingana na soko kuna wakati inafika Elfu 70Tsh sasa kuona tena hiii 1M kwa 1kg ikanishangaza.

Naomba mwenye ufafanuzi juu ya hili anisaidie kama ni fursa kweli niichangamkie🙏
 
nipo Njombe now mkuu na hao watu niliwatembelea kutafuta ubuyu tu ila kwa maelezo yao na nikaongeza na yangu siwezi kusita kusema hao ni MR KUKU WATARAJIWA MKUU kama unataka kuwekeza Njombe wee njoo ulime parachichi tu huku kwingine ni kuzugana tu.
 
Kweli kaka, nimekuwa nikipata mashaka sana juu ya matangazo yao na uhalisia ulioko katika wizara ya Kilimo na ufugaji kwamba wizara imeshindwa kutoa tamko kwa wakulima kuchangamkia hii fursa
 
Ndio hivyo mkuu kilimo chenye tija now kwa Njombe ni parachichi tu na watu wanakuja kwa wingi kuwekeza mno japo pia panahitaji umakini wa kununua ardhi.
 
Vanila 1mil ni bei ya 2018. Vanilla iliyokauka.
Na ni bei ambayo haijawahi jirudia tena.

Ukiambiwa Vanilla Kagera ni 60,000/= basi zidisha kwa 10, unapata 600,000/=. Hiyo ndio inakuwa bei ya Vanilla iliyokaushwa.

Kwa ujumla Vanilla iliyokaushwa ni mara 10 ya bei ya Vanilla mbichi.

Njombe Vanilla haitokaa istawi itoe matokeo kama wanavyotaka Vanilla Village. Maana Vanilla haitaki baridi kali kama ya Njombe.

Watu wa Morogoro, Pwani, n.k wana fursa ya kulima Vanilla ya kutosha na sio Njombe.
 
Huenda kweli hilo zao lina bei nzuri...lakini sasa kama watafanikiwa kuhamasisha uzalishaji wa zao kwa wingi sokoni bei itabaki hiyo hiyo?.
 
nipo Njombe now mkuu na hao watu niliwatembelea kutafuta ubuyu tu ila kwa maelezo yao na nikaongeza na yangu siwezi kusita kusema hao ni MR KUKU WATARAJIWA MKUU kama unataka kuwekeza Njombe wee njoo ulime parachichi tu huku kwingine ni kuzugana tu.
Nimewaatukia mapema Sana nasubiri muda
 
Mimi nataka kujua tu hiyo vanilla ina matumizi gani mpaka bei iwe hivyo au mambo ya kuongeza nguvu na maumbile kama ilivyo kwa faru wanavyotoweka kila uchwao.
 
Vanila 1mil ni bei ya 2018. Vanilla iliyokauka.
Na ni bei ambayo haijawahi jirudia tena.

Ukiambiwa Vanilla Kagera ni 60,000/= basi zidisha kwa 10, unapata 600,000/=. Hiyo ndio inakuwa bei ya Vanilla iliyokaushwa.

Kwa ujumla Vanilla iliyokaushwa ni mara 10 ya bei ya Vanilla mbichi.

Njombe Vanilla haitokaa istawi itoe matokeo kama wanavyotaka Vanilla Village. Maana Vanilla haitaki baridi kali kama ya Njombe.

Watu wa Morogoro, Pwani, n.k wana fursa ya kulima Vanilla ya kutosha na sio Njombe.
Kwa hiyo research imefanyika vibaya, ni kwel matokeo yatakuwa hayaridhishi
 
Tanzania Nchi Ngumu Sana
Watu Wamepigwa Sana Walimu Wastaafu Mpaka Millions 29
Serikali Ya Mkoa Imeingilia Kati, Hakuna Lolote Hapo
Ukiitiwa Fursa Ujue Wewe Mwenyewe Ndiyo Fursa

Mzilankende Alisema Kujenga Pembeni Ya Barabara Ni Kuufuata Umasikini.
DECI
Mr Kuku
Vanilla Village
Ni Ndugu Moja Hao
 
Wadau poleni na majukumu

Baada ya kipindi kirefu toka rafiki yangu anipe story juu ya zao la vanilla huko kwao Kagera na jinsi linalindwa haswa wakati wa kuvuna nilipata shauku ya kujua zaidi lakin kutokana na majukumu mengine sikuweza kufuatilia sana.
Ila kwa muda wa miezi mitatu sasa nimekuwa nikisikia matangazo kwenye Tv kuhusu Vanilla village huko Njombe na kinachonivutia na kuniogopesha pia ni juu ya bei 1kg/1M yaan hiyo hela kwa 1kg inaniogopesha sana kwan kwa maelezo ya awali niliambiwa kulingana na soko kuna wakati inafika Elfu 70Tsh sasa kuona tena hiii 1M kwa 1kg ikanishangaza.

Naomba mwenye ufafanuzi juu ya hili anisaidie kama ni fursa kweli niichangamkie[emoji120]
Upigaji
 
Vanilla kuuzwa kg 1 milioni Ni utapeli..
Bukoba tumelima vanaila miaka mingi Sana..Bei kwa kilo sio zaidi ya elfu 60..
Hiyo bei ya elfu 60 ni ya mwaka gani? Wenzio msimu wa mwaka huu tumeuza kwa elfu 30 na waliochelewa waliuza kwa elfu 25. Wengine waliuza kwa mkopo mpaka leo bado wanadai, hawajalipwa. Au wewe mwenzangu upo Kagera ipi?[emoji2][emoji2]

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Sasa mbona nilileta uzi sijajibiwa jamani kumbe bei ya kagera ni 30K? Mi naitaka hio Vanilla jamani. Naweza ipata hata kilo 10 tu? Iliokauka vizuri yani.
 
We mgeni hapa JF ? Kuna mada ya hao jamaa ilishajadiliwa Sana. Hamna kitu hapo piga chini. ..huyo Ni Mr kuku style. Badae msije kulia Lia hapa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom