Hali ya vijana wa Madagascar unaijua ndugu?
Nakumbuka miaka ya 92 ndo zao Hilo lililetwa Kagera na kilo moja ilianzia kumi elf, ikapanda hadi 20 elf na sasa ni laki mbili
Watu walilima sana na mwisho wa siku bei ikawa sio rafiki na kukatisha tamaa.
Kilimo chenyewe kilikuwa ni subsistence farming. Kiukweli tatizo kubwa la vanilla linaanzia kwa wanunuzi, kwani wanapunjwa sana, na pia ina grade zake km madini.
Kwenye kilimo ni kweli huchukua miaka 3-5 na ikikomaa basi huwa kama maharage na inatakiwa kukaushwa.
Suala kubwa la kukatisha tamaa ni kuwa endapo kutakuwa na kuku, panyabuku, mvua nyingi sana, dawa na uangalizi mdogo pindi inapoanza kuzaa na hadi kukaribia kukomaa basi Muda wowote mzizi au zao lenyewe huoza Bila kujali stage gani imefika.
Kwa kifupi inahitajika iwapo utajitoa katika zao la vanilla basi ni kama unavyoenda kutafuta madini. Na tatizo ni kutokuwepo kwa wataalam wa zao Hilo na hvyo kupandwa Bila kufuata vigezo na masharti.
Kushuka mara kwa mara kwa soko ndo ilipelekea watu kukata tamaa. Maringo na kutokuwepo kwa bei elekezi napo ni tatizo.
Kwa sasa kutokn na kuongezeka kwa viwanda vingi vinavyohitaji bidhaa hvy na uhaba wa wakulima kulima zao Hilo au kupunguza au demand kuwa kubwa imeipa heshima zao Hilo kipindi ambacho wakulima imewashtua na tatizo si zao la kupanda leo kesho ukavuna.
Kwa wale wanaopenda kwenda kulima zao Hilo, ujitoe muhanga kwani zao Hilo linahitaji hasubuh hadi jioni uwepo shambani, kwani wadudu, au ndege au kushindwa kuprune kwa baadhi ya matawi kwa siku chache tu zao Hilo litakuwa hasara kwao. Hata kwenye mitandao na mengineyo weka pembeni kwa miaka hyo, utafanikiwa