VAR hatuna basi tutumie TV re-play viwanjani kwa Sasa

VAR hatuna basi tutumie TV re-play viwanjani kwa Sasa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Video Assisted Referees (VAR) hatuna kwanini tusianzie na tv re-play (slow motions) viwanjani kwa baadhi ya matukio kama uhalali wa magoli na offsides? Goli la Konkoni kwenye mechi ya Yanga vs KMC nusura lilete dhahama pale kiwanjani. Na yapo matukio mengine ambayo kwa wanaoangalia replay wako na wakati mzuri wa kuyaona kuliko mwamuzi kiwanjani.
 
Goli la tatu alilofungwa KMC ,Simba au Yanga wanawezafungwa goli lile ligi kuu na mechi ikaendelea? Kwanza mshika kibendera atathubutu kusema goli?
Tunaosema ligi yetu inakuwa lazima tukerwe pia na matukio yanayonyima haki viwanjani. Timu Sasa zinasajili wachezaji 12 wa kigeni kwa gharama kubwa sana, kunyimwa haki kipumbavu au kwa bahati mbaya lazima tufanye kila jitihada ya kupunguza hilo
 
Hati Miliki Ya VAR Technology Hahiruhusu Kitu Kama Hicho Kutumia Video Re-play Kama Mbadala Wa VAR.

VAR Ni Kama Bidhaa Hivyo Unatakiwa Kununua Ili Itumike Viwanjani Na Sikutafuta Njia Nyingine Inayoshabiana Na VAR.
 
Video Assisted Referees (VAR) hatuna kwanini tusianzie na tv re-play (slow motions) viwanjani kwa baadhi ya matukio kama uhalali wa magoli na offsides? Goli la Konkoni kwenye mechi ya Yanga vs KMC nusura lilete dhahama pale kiwanjani. Na yapo matukio mengine ambayo kwa wanaoangalia replay wako na wakati mzuri wa kuyaona kuliko mwamuzi kiwanjani.
Ni vema tukaeleweshana ili siku nyingine usije na vioja kama hiki.
Teknolojia yoyote inayotumika kwenye maamuzi ya kisoka lazima iwe imepitishwa na FIFA kupitia IFAB.
Hakuna popote duniani teknolojia ya video replay imethibitishwa na IFAB kuwa njia ya kifikia maamuzi uwanjani.

Kwa maana hiyo, haiwezekani njia hiyo kutumika kwenye nchi ambazo ni mwanachama wa FIFA.
Kuhusu suala la Jana pale Chamazi, kanuni zinasema Mwamuzi akishaamua Jambo uwanjani maamuzi yake ndo ya mwisho. Ukiirudia video ya lile goli la 3 la Yanga halina mashaka zaidi ya ubishi wa kawaida wa Wachezaji kutokubali kushindwa.

Bega la kipa Maseke liko kwenye mstari wa goli upande wa ndani ya wavu, halafu mpira aliodaka uko begani si kifuani. Ukimwangalia Mwamuzi Msaidizi No.2 mara tu mpira ule ulipovuka mstari alinyoosha kibendera juu na kurudi Kati. Wakati mwingine Mechi inaweza kuvunjika sababu tu ya ukorofi wa timu na si mazingira ya tukio.

Tuliambiwa Azam iligoma kuendelea na mchezo wa kirafiki Tunisia baada ya beki wao Manyama kuvunjwa mkono wakiwa wanaelekea kufungwa goli 4. Lakini mchezaji huyohuyo alicheza Mechi ya Nusu fainali ya Ngao ya Jamii siku 9 baadaye. Mkono umefungwa POP mfupa ukaunga ndani ya siku 5 mchezaji akafanya mazoezi na Kwa tayari Kwa Mechi ndani ya siku 4 mbele.
 
Ni vema tukaeleweshana ili siku nyingine usije na vioja kama hiki.
Teknolojia yoyote inayotumika kwenye maamuzi ya kisoka lazima iwe imepitishwa na FIFA kupitia IFAB.
Hakuna popote duniani teknolojia ya video replay imethibitishwa na IFAB kuwa njia ya kifikia maamuzi uwanjani.
Kwa maana hiyo, haiwezekani njia hiyo kutumika kwenye nchi ambazo ni mwanachama wa FIFA.
Kuhusu suala la Jana pale Chamazi, kanuni zinasema Mwamuzi akishaamua Jambo uwanjani maamuzi yake ndo ya mwisho. Ukiirudia video ya lile goli la 3 la Yanga halina mashaka zaidi ya ubishi wa kawaida wa Wachezaji kutokubali kushindwa. Bega la kipa Maseke liko kwenye mstari wa goli upande wa ndani ya wavu, halafu mpira aliodaka uko begani si kifuani. Ukimwangalia Mwamuzi Msaidizi No.2 mara tu mpira ule ulipovuka mstari alinyoosha kibendera juu na kurudi Kati. Wakati mwingine Mechi inaweza kuvunjika sababu tu ya ukorofi wa timu na si mazingira ya tukio. Tuliambiwa Azam iligoma kuendelea na mchezo wa kirafiki Tunisia baada ya beki wao Manyama kuvunjwa mkono wakiwa wanaelekea kufungwa goli 4. Lakini mchezaji huyohuyo alicheza Mechi ya Nusu fainali ya Ngao ya Jamii siku 9 baadaye. Mkono umefungwa POP mfupa ukaunga ndani ya siku 5 mchezaji akafanya mazoezi na Kwa tayari Kwa Mechi ndani ya siku 4 mbele.
Goli la Yanga si tatizo. Tatizo ni hizi sintofahamu za marefa na udhaifu ambao wamekuwa wakiuonyesha viwanjani. Tunazitatua vipi iwapo hatuwezi kuwa na VAR.
 
sidhani kama ina ufanisi kama VAR
Kwavyovyote vile haiwezi kuwa na ufanisi kama VAR lakini ni Bora kuliko kutegemea waamuzi pekee viwanjani. Ni heri duni kuliko hakuna kabisa.

Kule kijijini Kuna watu wanalima kwa ng'ombe na punda, lakini ni heri kuliko wanaolima kwa jembe la mkono ingawa
Kwa hiyo lile lilikuwa ni goli, au siyo goli?
Lilikuwa goli halali kabisa hasa kwasisi tuliokuwa tunaangali re-play majumbani. Kama asingekuwa mshika kibendera refa alishalikataa.
 
Marefa wanachezesha mechi kama vile wamepewa maagizo na viongozi ni bahati sana kwa timu nje ya Simba na Yanga maamuzi ya refa yakawabeba.
 
Kwavyovyote vile haiwezi kuwa na ufanisi kama VAR lakini ni Bora kuliko kutegemea waamuzi pekee viwanjani. Ni heri duni kuliko hakuna kabisa.

Kule kijijini Kuna watu wanalima kwa ng'ombe na punda, lakini ni heri kuliko wanaolima kwa jembe la mkono ingawa

Lilikuwa goli halali kabisa hasa kwasisi tuliokuwa tunaangali re-play majumbani. Kama asingekuwa mshika kibendera refa alishalikataa.
kwani huu utaratibu ulikuwepo ?
 
Mkuu FIFA na CAF hawaruhusu mambo ya reply za tv,ni VAR tu zinatumika na wao ndo wamiliki,ndo maana hawataki mambo mengine zaidi ya VAR
 
Mkuu FIFA na CAF hawaruhusu mambo ya reply za tv,ni VAR tu zinatumika na wao ndo wamiliki,ndo maana hawataki mambo mengine zaidi ya VAR
Hiyo ni kanuni namba ngapi ya FIFA? Siku hizi Kuna makampuni mengi ya kubet, marefa wanapata majaribu na mashinikizo mengi sana kutoka kwa waliobet. Refa pia ni binadamu kama wengine, ana njaa zake na timu yake anayoipenda, yote haya yanaweza kuhatarisha maamuzi ya mwamuzi.

Kama ingekuwa FIFA inakataza basi ingesema hakuna mechi kuchezwa bila VAR. Hayo ni mawazo yako wewe.
 
Goli la Yanga si tatizo. Tatizo ni hizi sintofahamu za marefa na udhaifu ambao wamekuwa wakiuonyesha viwanjani. Tunazitatua vipi iwapo hatuwezi kuwa na VAR.
Namna mpira wetu unavyoendelea kupiga hatua Iko siku mpira wetu huu utasababisha madhara na maafa makubwa sana viwanjani na mitaani. Timu sinasajili wachezaji wakubwa, zinaenda pre-season na zinafanya kila aina ya uwekezaji ili kuepuka kufungwa. Haitawezekana kuona "human error" ziyeyushe jitihada zao hizi kwa kuwatengenezea matokeo. mark my words....
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom