Ni vema tukaeleweshana ili siku nyingine usije na vioja kama hiki.
Teknolojia yoyote inayotumika kwenye maamuzi ya kisoka lazima iwe imepitishwa na FIFA kupitia IFAB.
Hakuna popote duniani teknolojia ya video replay imethibitishwa na IFAB kuwa njia ya kifikia maamuzi uwanjani.
Kwa maana hiyo, haiwezekani njia hiyo kutumika kwenye nchi ambazo ni mwanachama wa FIFA.
Kuhusu suala la Jana pale Chamazi, kanuni zinasema Mwamuzi akishaamua Jambo uwanjani maamuzi yake ndo ya mwisho. Ukiirudia video ya lile goli la 3 la Yanga halina mashaka zaidi ya ubishi wa kawaida wa Wachezaji kutokubali kushindwa. Bega la kipa Maseke liko kwenye mstari wa goli upande wa ndani ya wavu, halafu mpira aliodaka uko begani si kifuani. Ukimwangalia Mwamuzi Msaidizi No.2 mara tu mpira ule ulipovuka mstari alinyoosha kibendera juu na kurudi Kati. Wakati mwingine Mechi inaweza kuvunjika sababu tu ya ukorofi wa timu na si mazingira ya tukio. Tuliambiwa Azam iligoma kuendelea na mchezo wa kirafiki Tunisia baada ya beki wao Manyama kuvunjwa mkono wakiwa wanaelekea kufungwa goli 4. Lakini mchezaji huyohuyo alicheza Mechi ya Nusu fainali ya Ngao ya Jamii siku 9 baadaye. Mkono umefungwa POP mfupa ukaunga ndani ya siku 5 mchezaji akafanya mazoezi na Kwa tayari Kwa Mechi ndani ya siku 4 mbele.