Umewahi kuchezesha mpira, Hata hii ya makaratasi? Kwasababu ungekua umewahi ungejua kua matendo mengine nikawaida mwamuzi anahukumu vitendo vitatu uwanjani, kabla ya kitendo, wakati wa kitendo na baada ya kitendo.
Sasa kwa hali hiyo sio wakati wote maamuzi yatakua sahihi kwasababu maamuzi yanaweza kuathiriwa na mwendo kasi wa tukio, umbali wa tukio na angle ya tukio. Kupitia sababu zote hizo anachotakiwa kufanya refa nikuhukumu kwanza tukio ndio hayo mengine yakushauriwa kuhusu alichokihukumu yanafuata.
Uko kwenye chumba cha VAR wako marefa ambao wanamshauri mwamuzi wa kati baada ya kupitia marejeo ya camera kwenye angle zote ila maamuzi ya mwisho yanabaki kua yamwamuzi wa kati kwajinsi atakavyotafsiri tukio.
Wewe unaona wanakosea kwasababu unatazama marejeo ya video lakini kwa kasi ya matukio ya uwanjani sio kitu rahisi kuhukumu matukio yote kwa usahihi.Na mpira sio mchezo wa ukamilifu bali makosa.