Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lengo la kuileta tech hii lilikua zuri isipokua kumekuwepo mapungufu au dosari katika mfumo huu,nini kilitakiwa
1)Var ilitakiwa iwe ina operate yenyewe kama mashine katika maamuzi kwa 95% ikishirikiana na mwamuzi wa Kati kwa 5%
2)Viatu vyote vya wachezaji pamoja na Lines zote uwanjani viwe installed na sensor,hata ikibidi wachezaji wavalishwe signals ili ikitokea mchezaji kawa offside mashine iwashe taa nyekundu na kumtaarifu refa direct kua ni off side kabla hata goli kuingia nyavuni au hata mchezaji haja shoot
Warekebishe mambo hayo kulikoni ilivyo sasa goli linafungwa ati binadamu kwa utashi wao waamue kulihakiki au kukaushia,yaani kutegemea na mapenzi yao,au kwanza goli likifungwa wanaanza kuongea na refa muda mrefu kushauriana!
Hapo Var inakosa maana kama wameamua Var itumike basi zifanye kazi ktk Auto mode na si manual
Ifikie pahala Var system ndio ituambie tena kwa haraka goli au si goli,Offside au sio offside,Faul au si faul....na si kutumia watu wanne hivi ndio wawe wanaamua maamuzi mbaya zaidi mpira tunauona wote
Kiukweli Var bila maboresho ni majanga. Var ifanye kazi na refa direct.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni mapungufu yake yenyewe haina shida
Kuja kwa Var Tanzania na maeneo mengine ya dunia hilo nalo ni pungufu ambalo Fifa walirekebishe haraka
Kama Var inatumika Uk na Europe basi inabidi itumike dunia nzima ili kuweka uwiano sawa
Ligi moja kutumia Var nyingine kutotumia ni kasoro kubwa sana haijengi usawa baina ya timu zitumiazo Var na zisizotumia
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli lakini ziwepo machine kwenye var si binadamu ambao wanaamua jambo pale tu wanapotaka waovar Ni msaidizi wa mwamuzi sio mwamuzi